Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres atoa sababu za kuikubali Arsenal

Muktasari:

  • Gyokeres amesaini mkataba wa miaka mitano na Arsenal, ambao utamwezesha kukunja karibia Pauni 300,000 kwa wiki.

London, England. Staa mpya wa Arsenal, Viktor Gyokeres ameweka wazi sababu ambazo zilimfanya aichague timu hiyo na kukataa ofa nyingine zilizowasilishwa mezani katika dirisha hili.

Fundi huyo raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 27, amekamilisha uhamisho wa Pauni 63.5 milioni kwenda Arsenal akitokea Sporting Lisbon mapema wikiendi iliyopita.

Hata hivyo, kabla ya kukubali dili hilo, Gyokeres alipokea ofa nyingine ikiwamo ile ya Manchester United ambayo alitabiriwa kuwa ataikubali kutokana na uhusiano uliopo kati yake na kocha wa mashetani wekundu hao, Ruben Amorim, lakini bado alikataa.

Baada ya kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Arsenal, Gyokeres alifunguka kuhusu uamuzi wake akisema: "Nilihisi tu kwamba hii ilikuwa klabu sahihi kwangu. Kile nilichosikia kutoka kwa Mikel Arteta na Andrea Berta wakati nilipokuwa nazungumza nao, pamoja na kile nilichokiona kwa miaka ya hivi karibuni, jinsi walivyokuwa wakicheza soka kilinishawishi."

"Nilipokutana nao uwanjani msimu uliopita, nilihisi kabisa kuwa ni timu imara sana na ilikuwa vigumu sana kucheza dhidi yao. Hilo ndilo lililonisukuma kuichagua Arsenal na bila kusahau historia kubwa ya klabu hii na mashabiki wake lukuki. Imenifurahisha sana kuona sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki hata kabla sijawasili. Hicho ndicho kinachofanya hii klabu kuwa maalum. Itakuwa ni furaha kubwa kuwaona kiwanjani."

Gyokeres amesaini mkataba wa miaka mitano na Arsenal, ambao utamwezesha kukunja karibia Pauni 300,000 kwa wiki.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Brighton, Swansea na Coventry amepewa jezi namba 14 ambayo iliwahi kuvaliwa na gwiji Thierry Henry.

Baada ya kuanza mazoezi wiki hii, anaweza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Arsenal Alhamisi ijayo dhidi ya Tottenham katika mechi ya kirafiki itakayopigwa visiwa vya Hong Kong.

Kocha wa Arsenal, Arteta baada ya kukamilika kwa usajili huo alisema: "Tuna furaha kubwa kumpokea Viktor Gyokeres katika klabu yetu. Ameonyesha uimara mkubwa katika kiwango chake cha uchezaji. Idadi ya mabao aliyofunga inajieleza yenyewe. Ana sifa nyingi ni mwepesi, mwenye nguvu katika eneo la mbele na ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Ana uwezo mzuri wa kubadilisha nafasi kuwa mabao na anajua kujipanga vizuri kwenye eneo la hatari, jambo linalomfanya kuwa tishio la kudumu."