Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland alivyoikatili Brazil Kombe la Dunia

NORWAY Pict

Muktasari:

  • Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila kufungana, straika wa Norway, Erling Haaland  aliibuka shujaa wa mchezo kwa kufunga mabao mawili katika dakika kumi za mwisho na kuiongoza timu hiyo kutinga robo fainali.

Brazil imeaga fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kufungwa mabao 2-1 na Norway katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa kwenye Uwanja wa New York/New Jersey, Marekani.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila kufungana, straika wa Norway, Erling Haaland  aliibuka shujaa wa mchezo kwa kufunga mabao mawili katika dakika kumi za mwisho na kuiongoza timu hiyo kutinga robo fainali.

Haaland alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 80, baada ya kumzidi ubabe beki Gabriel Magalhães katika pambano lao la ana kwa ana lililodumu kwa muda wote wa mechi.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City alionyesha kwa mara nyingine kuwa hahitaji kugusa mpira mara nyingi ili kuamua matokeo ya mchezo. Bao lake la sita katika Kombe la Dunia lilitokana na mguso wake wa 21 pekee, likiiweka Brazil kwenye hali ya kukata tamaa ambayo hata kocha Carlo Ancelotti hakuweza kuibadili.

Baadaye aliongeza bao la pili dakika ya 90 likiwa la saba kwake katika fainali za mwaka huu akiachia shuti kali kutoka umbali wa takribani yadi 20 lililojaa moja kwa moja kwenye kona ya mbali, na kuhitimisha safari ya Brazil katika mashindano hayo. Bao hilo lilikuja baada ya kugusa mpira mara 26 pekee.

Mbali na Haaland, kipa Orjan Nyland alikuwa nguzo muhimu ya ushindi wa Norway. Aliokoa penalti ya mapema ya Bruno Guimarães dakika ya 14, akamzuia Vinícius Júnior na Rayan wasifunge, kabla ya kuzuia kwa ustadi mpira uliokuwa ukielekea wavuni kutoka kwa mwenzake Kristoffer Ajer ambao ungeweza kuwa bao la kujifunga.

Brazil ilifanikiwa kupata bao moja kupitia Neymar Jr kwa penalti dakika ya 90+10, lakini halikutosha kuizuia Norway kuandika ushindi wa kihistoria. 

Kwa ushindi huo, Norway imefuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya kwanza, huku Brazil ikiondolewa mapema kwenye mashindano hayo licha ya kuingia ikiwa miongoni mwa timu zilizopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.