Haaland, Dias na Mbappe wafukuzia rekodi
Muktasari:
- Michezo ya Ligi uko Ulaya imechezwa huku rekodi zikiendelea kufukuziwa, Aguero, Shearer na Robbier Fowler, matatani kwa Haaland.
LONDON, ENGLAND: Ligi mbalimbali zimeendelea kupigwa Barani Ulaya ambapo kwenye Ligi pendwa ya England maarufu kama EPL ilichezwa michezo tofautu tofauti huku mchezo wa mapema ulikuwa kati ya Arsenal dhidi ya Wolverhampton uliopigwa saa 8:30 mchana wenyewe wakiita “The Lunch time kick off”, wakati ikishuhudiwa rekodi mbili zikiwekwa.
Bukayo Saka amekuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi za magoli (assist) kwenye michezo mitatu ya mwanzo tangu alipofanya hivyo Thierry Henry msimu wa mwaka 2004/2005.
Declan Rice alionyeshwa kadi nyekundu dakika 49 ya mchezo ikiwa ndiyo kadi ya kwanza tangu alipoanza Maisha yake ya soka.
Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Manchester City dhidi ya West Ham, Erling Haaland alifanikiwa kufunga mabao matatu yaani “Hat Trick” ikiwa ni mara ya pili kwenye michezo mitatu ya mwanzo tangu alivyofanya hivyo Paul Jewell wa Bradford msimu wa mwaka 1994/95
Haaland anafikisha jumla ya Hat trick nane tangu alipotua England akishika nafasi ya nne nyuma ya kinara Sergio Kun Aguero mchezaji wazamani wa Man City mwenye Hat trick 12, Alan Shearer mchezaji wa zamani wa Man United akiwa nafasi ya pili na Hat trick 11, Pamoja na Robbie Fowler mchezaji wazamani wa Liverpool akiwa nafasi ya tatu na Hat trick tisa.
Kwenye mchezo kati ya Manchester United na Liverpool, Luis Dias anakuwa mchezaji wa pili kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza katika Uwanja wa Old Trafford tangu alivyofanya hivyo Mohamed Sarah msimu wa mwaka 2021/2022.
Mo Sarah alifunga bao lake la kumi katika michezo nane kwenye mashindano yote aliyocheza uwanja wa Old Trafford akiwa na Liverpool, hii inamfanya anakuwa mchezaji wa pili kufunga mabao kumi kwenye uwanja mmoja wa ugenini, tangu alivyofanya hivyo mchezaji wa zamani wa Man United Alan Shearer msimu wa mwaka 1992-93 kwenye uwanja wa Elland Road dhidi ya Leeds United.
Huko Hispania kwenye La Liga mchezaji wa FC Barcelona Raphael Dias maarufu kama “Raphinha” alifunga mabao matatu (hat trick) ikiwa ni mara ya kwanza akiwa na Barcelona, huku akiifikia rekodi ya kufunga mabao matatu kwenye michezo ya mwanzoni tangu Lionel Messi alivyofanya hivyo mwaka 2004.
Mabao mawili aliyofunga Kylian Mbappe dhidi ya Real Betis yamemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo kama mchezaji mpya wa Madrid, tangu Christiano Ronaldo alivyofanya hivyo mwaka 2009 akitokea Manchester United.