Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali ilivyo Uwanja wa Benjamin Mkapa, ufunguzi CHAN ukikaribia

Muktasari:

MIONGONI mwa kauli alizozitoa kipa wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Aishi Manula aliyeomba wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwasapoti katika mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan), dhidi ya Burkina Faso.

MIONGONI mwa kauli alizozitoa kipa wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Aishi Manula aliyeomba wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwasapoti katika mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan), dhidi ya Burkina Faso.

Kauli hiyo Manula aliitoa jana wakati anazungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mechi hiyo: "Tupo katika ardhi ya nyumbani, Watanzania waje ili tujisikie nguvu ya kupambana."

Taifa Stars inacheza dhidi ya Burkina Faso, mechi hiyo itayopigwa saa 2:00 usiku, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Watanzania wameitikia wito huo kwa kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuisapoti timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itakayokuwa na mechi dhidi ya Burkina Faso.

Nyomi ya watu imejaa nje ya uwanja ikisubiri saa 2:00 ambapo mechi hiyo itachezwa, huku wengine wakiwa sehemu ya vinywaji na chakula wakipata huduma.

Mbali na hao, wapo ambao wanatembea, baadhi wakiwa wamejichora rangi za bendera ya Tanzania, wengine wakiwa wamebeba vikapu vilivyoandika ujazo wa mabao wakiamini bendera ya taifa inakwenda kupeperushwa vyema.

BIASHARA

Kupitia michuano ya CHAN baadhi ya Watanzania wamenufaika na kufanya biashara za vyakula, vinywaji,matunda na bidhaa mbalimbali.

Mmoja wa mama lishe aliyejitambulisha kwa jina la Aisha amesema:" Biashara inaenda vizuri, naamini hadi michuano iishe nitakuwa nimenufaika na kujipatia kipato."

ULINZI

Tofauti na ilivyozoeleka ikichezwa dabi ya Simba na Yanga ambapo kunakuwa na mipaka ya kukaa mashabiki wakisubili kuingia uwanjani, awamu hii  wamewekwa mbali zaidi na geti kubwa la kuingilia uwanjani.

Uzio wa kuwatenganisha mashabiki hao na geti la kuingilia uwanjani umesogezwa nyuma zaidi pamoja na sehemu za maegesho ya usafiri kwa maana ya magari na bodaboda zipo mbali.

Pamoja na hayo kufanyika ulinzi umeimarishwa  kuna askari wapo ndani ya uzio na wengine wapo nje, huku hali ya utulivu ikiwa imetawala, stori za hapa na pale za wengi wao wakisubili kuona Stars itafanya kitu gani katika mechi ya ufunguzi na Burkina Faso