Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya hapa makundi ya Klabu Bingwa Dunia

Muktasari:

  • Inter Miami ya Lionel Messi itakutana na Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa ufunguzi katika Uwanja wa Hard Rock, Miami.

Miami, Florida. Droo ya Klabu Bingwa Dunia imechezeshwa jana ambapo Mabingwa watetezi Manchester City watakutana na Juventus katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la Klabu huku Chelsea wakikutana na timu ya Flamengo kutoka Brazil.

Man City ambao waliifunga Fluminense kutoka Brazil kwenye fainali za msimu uliopita ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza 2023, wataanza kutetea taji lao dhidi ya Wydad ya Morocco na pia kucheza na Al Ain kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu katika Kundi G.

Inter Miami ya Lionel Messi itakutana na Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa ufunguzi katika Uwanja wa Hard Rock, Miami.

Chelsea mabingwa wa fainali ya 2021, walipangwa pia pamoja na Club Leon ya Mexico na Esperance Sportive de Tunisie ya Tunisia katika Kundi D.

Real Madrid ambao walinyakua Kombe la Dunia la Klabu za FIFA kwa mara ya tano 2022, watacheza mechi ya kwanza dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Saudi, Al-Hilal, ambayo kwa sasa anachezea Staa wa Brazil Neymar Jr.

Kwingineko, Paris St-Germain walipangwa dhidi ya Atletico Madrid katika Kundi B, huku Bayern Munich wakikutana na Benfica katika mechi nyingine ya hatua ya makundi kati ya timu za Ulaya.


Makundi ya Kombe la Dunia la Klabu za FIFA 2025

Kundi A: Palmeiras, FC Porto, Al Ahly, Inter Miami

Kundi B: Paris St-Germain, Atletico Madrid, Botafogo, Seattle Sounders

Kundi C: Bayern Munich, Auckland City, Boca Juniors, Benfica

Kundi D: Flamengo, Esperance Sportive de Tunisie, Chelsea, Club Leon

Kundi E: River Plate, Urawa Red Diamonds, Monterrey, Inter Milan

Kundi F: Fluminense, Borussia Dortmund, Ulsan, Mamelodi Sundowns

Kundi G: Manchester City, Wydad, Al Ain, Juventus

Kundi H: Real Madrid, Al Hilal, Pachuca, Salzburg

Awali, mashindano haya yalikuwa yanafanyika kila mwaka na kushirikisha timu saba bora kutoka mabara sita (AFC, CAF, Concacaf, Conmebol, OFC, na UEFA) lakini sasa yatakuwa na timu 32 na kufanyika kila baada ya miaka minne.

Kila timu itacheza mara moja na timu nyingine katika kundi lake, timu mbili zitakazo maliza nafasi za juu kutoka kila kundi zitafuzu hatua ya mtoano ambapo hakutakuwa na mchezo wa kuwania nafasi ya tatu na mchezo wa fainali utafanyika tarehe 13 Julai 2025.

Mashindano haya yataanza kutimua vumbi Juni 15, hadi Julai 13, 2025. Viwanja 12 vitatumika ambapo mchezo wa ufunguzi utafanyika kwenye uwanja wa Hard Rock uliopo Miami, Florida na mchezo wa fainali uatapigwa kwenye uwanja wa MetLife uliopo New Jersey, Marekani, ikiwa ni maandalizi kuelekea Kombe la Dunia la 2026.