Ibenge apewa kibarua kizito Sudan

Thursday August 04 2022
ibenge pic
By Leonard Musikula

Klabu ya Al Hilal ya Sudan inatarajiwa kumtangaza rasmi kocha wao mpya Florent Ibenge aliyewahi kuzinoa klabu za As Vita ya Congo na Rs Berkane ya Morroco baada ya kocha huyo kukubali mkataba wa miaka mitatu wa kikosi cha mabingwa hao wa Sudan

Baada ya msimu mmoja na nusu akiwa na Renaissance Berkane, taji la Kombe la CAF na Kombe la Enzi, Florent Ibenge amekubali kuanza changamoto mpya huku klabu hiyo ikimbebesha mtihani mzito wa kuhakikisha anaifikisha hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Hilal Omdurman alitangaza wikendi hii, kuwasili kwa Florent Ibenge karibu katika ardhi ya Sudan, kwa ajili ya kuanza safari yake mpya. Klabu hiyo itashiriki Ligi ya Mabingwa ya CAF ijayo, mashindano ambayo kocha wa Kongo anayafahamu vyema, baada ya kucheza mara kadhaa na AS Vita Club, na hata kufika fainali mwaka wa 2014.

Hata hivyo Viongozi wa timu hiyo wamekuwa na matumaini makubwa na kocha huyo kutokana na hadhi yake ya kuwa kocha mwenye uzoefu mkubwa nna mwenye rekodi kubwa ya utendaji ambapo pia inatazamwa  kuletea Hilal mwelekeo mwingine, haswa kwenye eneo la kutwaa mataji mbalimbali yta ndani na hata nje.


Taarifa kutoka Sudan zinasema kuwa kocha huyo tayari ameshawasili nchini Sudan  kujiunga na klabu ya Al Hilal huku pia winger Glody Lilepo kutoka AS Vita ya DR Congo aliyesajiliwa kwa dau la Sh 1.3 bilioni na klabu ya Al Hilal naye amewasili nchini Sudan.


Advertisement
Advertisement