Jenifer Kanumba mikononi mwa Billnass

Jenifer Kanumba mikononi mwa Billnass

Muktasari:

  • Msanii maarufu wa Bongomovie, Jenifer Kanumba mikononi mwa Billnass. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii huyo kuonekana katika video ya msanii huyo wa Bongofleva.

Msanii maarufu wa Bongomovie, Jenifer Kanumba mikononi mwa Billnass. Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya msanii huyo kuonekana katika video ya msanii huyo wa Bongofleva.

Jenifer ambaye jina lake halisi ni Hanifa Daudi, ameonekana katika video ya wimbo mpya wa Billnass unaitwa ‘Tatizo’ ambao kauachia jana Ijumaa Aprili 10, 2021.

Katika wimbo huo Jenifer amekuwa video vixen, na hii inakuwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo baada ya muda mrefu kujikita katika masuala ya uigizaji filamu.

Jenifer ni kati ya wasanii walioanza sanaa wakiwa na umri mdogo, ambapo marehemu Steven Kanumba ndiye aliyeibua vipaji vyao akiwa na mwenzake Patrick Moaka kujikuta akipachikwa jina la Jenifer Kanumba.

Kanumba aliweza kuwachezesha vilivyo katika filamu ya Uncle JJ na This is It na kujikuta wanajizolea mashabiki kibao wakubwa kwa watoto.

Tangu kufariki kwa Kanumba ni kama umaarufu wao ulipiotea na watu kutoendelea kuwatumia lakini kwa sasa wanaonekana tena katika tamthiliya ya Pazia.