Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jezi za Simba zauzwa Njombe

Muktasari:

Katika hali  ya kawaida jezi zilizotarajiwa kuuzwa kwa wingi mjini hapa ni za Yanga na wenyeji Njombe lakini Simba nayo imechomoza.

 Katika hali ya kushangaza, jezi za Simba zimeonekana kupata soko kubwa hapa mjini Njombe wakati ambapo timu ya Yanga ikijiandaa kuikabili Njombe Mji leo jioni.

Katika hali  ya kawaida jezi zilizotarajiwa kuuzwa kwa wingi mjini hapa ni za Yanga na wenyeji Njombe lakini Simba nayo imechomoza.

Miongoni mwa jezi za nyota wa Simba zinazouzika mjini hapa ni zenye majina ya Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi huku za Yanga zikipambwa na jina la Papy Kabamba Tshishimbi.

"Jezi za Simba zinauzika kwa kuwa nchi nzima timu hizi zina mashabiki, wengine wananunua za Yanga lakini siyo sababu ya kuacha za Simba. Jezi za Njombe bado hazipatikani sana," alisemba Muuzaji mmoja wa jezi maarufu kama Mbunge wa Yanga Manzese.