Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaizer Chiefs yamkomalia Nabi

Muktasari:

  • Wababe wa Soweto, Kaizer Chiefs wamerudisha tena majeshi kwa Nabi kwa mara ya pili baada ya msimu uliopita kwa lengo la kutaka kwenda kulinusuru jahazi.

Dar es Salaam. Klabu ya Kaizer Chiefs imeonyesha tena nia ya kutaka huduma ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi baada ya mwaka jana kumkosa.

Dili la Nabi kwenda Kaizer lilifeli baada ya kushindwana nao kwenye baadhi ya masharti kisha Molefi Ntseki kuchukua mikoba hiyo ambapo alidumu kwa miezi mitatu kabla ya kutimuliwa.

Nabi ambaye kwa sasa anaifundisha FAR Rabat ya Morocco aliyojiunga nayo Julai 2023 akitokea kwa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga.

Amakhosi wamehusishwa na majina kadhaa, ikiwamo Alexandre Santos raia wa Ureno ambaye ameachana na wababe wa Angola Petro de Luanda baada ya kushinda taji la Ligi Kuu Angola. 

Licha ya mazungumzo yaliyothibitishwa kati ya Santos na Kaizer, inafahamika kuwa Amakhosi hawatasonga mbele katika mazungumzo na kocha huyo kuchukua nafasi inayoshikilia Cavin Johnson.  

Johnson ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya vijana ya Kaizer kabla ya kupandishwa kwenye timu ya wakubwa baada ya Molefi Ntseki kutimuliwa baada ya siku 114 tu tangu Oktoba mwaka jana.

Kaizer inaonyesha zaidi nia ya kumtaka Nabi baada ya kumkosa msimu uliopita kutokana na kushindwana kwenye baadhi ya masharti.

Miamba hao wa Soweto, ambao wamemaliza kampeni za msimu wa 2023/24 katika nafasi mbaya ya 10 ikiwa ni rekodi mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo, sasa wako tayari kulipa fidia kwa AS FAR ili kununua kandarasi ya Nabi ambayo inaisha Juni 2025.

Iwapo mambo yataenda vizuri kwa Nabi, Kaizer wapo tayari kumruhusu Mtunisia kwenda na jopo la wafanyakazi wake wa usaidizi na ili kumsaidia kuunda upya kikosi ambacho kitakachoweza kurudisha siku za utukufu wa Amakhosi kufuatia msimu huu kuwa mbaya kwao.