Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaizer Chiefs yathibitisha kifo cha Luke Fleurs

Beki wa Kaizer Cheifs mwenye miaka 24, Luke Fleurs ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea SuperSport United Oktoba mwaka jana, amepigwa risasi na kuuawa wakati wa tukio la utekaji nyara huko Honeydew.

Inadaiwa kuwa Fleurs alikuwa katika kituo cha mafuta jana na ndipo walipofika watu kadhaa ambao walimtaka atoke nje ya gari lake. Kisha wanadaiwa kumpiga risasi na kuondoka. Chiefs wamethibitisha kifo cha beki huyo.

"Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kwamba mchezaji wa Kaizer Chiefs, Luke Fleurs alipoteza maisha jana usiku wakati wa tukio la utekaji nyara huko Johannesburg," ilisema taarifa ya klabu hiyo.

“Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia yake na marafiki katika wakati huu mgumu. SAPS inashughulikia suala hilo na maelezo zaidi yatawasilishwa kwa wakati ufaao. Roho yake mpendwa ipumzike kwa amani.”

Fleurs alianza kucheza soka la kulipwa akiwa Ubuntu Cape Town 2017, kabla ya kuhamia SuperSport United mwaka mmoja baadaye.

Aliondoka SuperSport mwaka jana, 2023 na kujiunga na Chiefs kama mchezaji huru.