Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kanuni iliyoleta refa Mmisri Kariakoo Derby hii hapa

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 79 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 78.

Homa ya pambano la watani wa Jadi Yanga na Simba inazidi kupamba moto siku mbili kabla ya mechi hiyo kuchezwa.

Uhondo wa Kariakoo Derby ya safari hii unachangiwa zaidi na hesabu za ubingwa ambazo kila timu inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili iweze kuondoka na taji la Ligi Kuu msimu huu.

Lakini kinachonogesha zaidi ni uteuzi wa marefa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuchezesha mchezo huo namba 184.

Hapana shaka kanuni ya 39(2) ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ndio imeipa nguvu kamati ya marefa ya TFF kuwateua marefa kutoka Misri kuchezesha mechi ya Ligi Kuu baina ya Simba na Yanga, keshokutwa Jumatano, Juni 25, 2025.

Kanuni hiyo inafafanua kwamba kamati inaweza kufanya uteuzi wa marefa tofauti na wale waliopo katika orodha ya mwanzoni mwa msimu.

“ Katika Orodha ya Waamuzi Teule wa Ligi Kuu kutakuwepo waamuzi wachache wa akiba kwa Ligi Kuu wanaoweza kujumuishwa kuchezesha michezo ya Ligi Kuu katika mazingira ya dharura au uwepo wa haja ya
kufanya hivyo kwa sababu zinazoaminika. 

Leo Jumatatu, Juni 23, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia, mechi ya watani wa jadi wa Ligi Kuu Tanzania Bara itachezeshwa na marefa kutoka nje ya nchi.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo muda leo imesema mchezo huo utaamuliwa na mwamuzi Amin Omar akisaidiwa na Mahmoud El Regal, Samir Mohamed wakati mwamuzi wa nne mezani akiwa Ahmed Elghandour wote kutoka Misri huku mtathimini waamuzi akipewa Alli Mohamed kutoka Somalia.

Hii inakuwa mara ya kwanza kihistoria kwa mchezo huo kuamuliwa na waamuzi kutokanje wakati timu hizo kubwa mbili zinapokutana kwenye mashindano ya ndani.

Rekodi zinaonyesha Omar amewahi kusimamia mechi mbili za mashindano ya Afrika kwa timu hizo mbili, ambazo zote hakuna timu iliyoshinda.

Omar alisimamia mchezo wa nyumbani wa Yanga dhidi ya Mamelodi msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi ikimalizika wa sare isiyo na mabao.

Mwamuzi huyo pia aliamua mchezo wa Horoya dhidi ya Simba, ambapo wekundu hao walilala kwa bao 1-0 ikiwa pia ni mechi ya Ligi ya mabingwa.

Katika msimu wa 2024/2025, refa Amin amechezesha idadi ya mechi 22 za mashindano tofauti ambapo ameonyesha idadi ya kadi 87.

Katika kadi hizo 87 ambazo refa Amin ameonyesha katika mechi 22 ambazo amechezesha katika msimu wa 2024/2025, kadi nyekundu ni moja na za njano 86.