Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kipigo, Slot asusia tuzo

Muktasari:

  • Liverpool ilimtuma balozi wa klabu, Gary McAllister, kuchukua tuzo kwa niaba kocha.

Meneja wa Liverpool, Arne Slot, alikosekana kabisa kwenye hafla ya utoaji tuzo licha ya kutangazwa kuwa Kocha Bora wa Mwaka na Chama cha Waandishi wa Habari England.

Slot alijitoa dakika za mwisho, siku moja tu baada ya kikosi chake kupigwa 3-0 nyumbani na Nottingham Forest, kipigo kilichoendelea kuonyesha hali ngumu ndani ya kikosi chake ambacho sasa kimeporomoka vibaya na kupoteza mechi nane kati ya 11.

Kwa kukosa kwake, Liverpool ilimtuma balozi wa klabu, Gary McAllister, kuchukua tuzo kwa niaba yake. Taarifa zinasema McAllister alikuwa Elland Road akishuhudia mechi ya Leeds dhidi ya Aston Villa, ndipo akapigiwa simu na kuombwa abadili ratiba mara moja.

McAllister aliwasomea wageni ujumbe mfupi wa Slot uliokuwa na samahani pamoja na shukrani, akisisitiza kuwa anajivunia sana kutwaa tuzo hiyo licha ya misukosuko ya sasa.

Miongoni mwa waliotunukiwa siku hiyo ni kocha wa Leeds Daniel Farke, kocha wa Wrexham Phil Parkinson, na kocha wa Newcastle Eddie Howe.

Mwaka jana, kocha wa Manchester United wakati huo, Erik ten Hag, ndiye alikuwa meneja mkubwa wa mwisho kuhudhuria hafla kama hiyo lakini cha kusikitisha, alifurahia tuzo siku chache kabla ya kufungashiwa virago na uongozi wa United.

Baada ya kipigo kutoka kwa Forest ambacho kimeweka rekodi mbaya kwa Liverpool kwa kukubali kipigo Anfield mara mbili mfululizo tangu 1978—Slot hakutaka kukwepa lawama.

“Ninawajibika moja kwa moja kwa matokeo haya, huwezi kuja na visingizio vya kutosha kwa hali tuliyonayo. Hatujafikia viwango vizuri kabisa, na jukumu ni langu,” alisema Slot.

Aliongeza kuwa timu imekuwa ikicheza vizuri katika mechi nyingi lakini inakosa nafasi muhimu, huku wapinzani wakifunga mabao mepesi yanowavuruga.

“Tunahitaji ile nguvu ya kupata bao la kwanza. Tukipata, mchezo unabadilika. Lakini tumekuwa tukipata kinyume chake tukifungwa kwanza na kujikuta tukiwa nyuma,” alisema.

Hata hivyo, Slot alisisitiza kuwa hali hiyo haiwezi kuendelea msimu mzima, ingawa akakiri wazi Liverpool wako katika kipindi kigumu kinachohitaji juhudi na umakini zaidi.