Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa kugomea medali, Azam FC yapigwa rungu na TFF

Muktasari:

  • Katika mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB iliyochezwa kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, Azam ilifungwa bao 1-0 na Simba.

Dar es Salaam. Azam FC imekumbana na rungu la adhabu kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia matukio yaliyotokea baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB ilipopoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Simba.

Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana jijini Dar es Salaam, ilipitia taarifa ya mchezo huo uliopigwa Julai 4, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, na kutoa uamuzi dhidi ya Azam pamoja na baadhi ya wahusika wa benchi la ufundi na wachezaji wake.

Klabu hiyo imetozwa faini ya Sh50 milioni kwa kosa la kugomea sherehe za kukabidhiwa zawadi ya mshindi wa pili baada ya mchezo huo wa fainali kuisha, adhabu inayohusisha kanuni ya 27:7 ya Ligi Kuu.

Uamuzi huo haukuishia hapo, kocha wa makipa, Roudy Mountaro, amefungiwa michezo minne na kutozwa faini ya Sh2 milioni kwa kumshambulia mwamuzi, huku kipa Zuberi Foba akifungiwa mechi tatu na faini ya Sh2 milioni kwa kosa hilohilo la kumshambulia mwamuzi baada ya filimbi ya mwisho.

Wakati huohuo, Kamati ya Mashindano ya TFF imewasilisha shauri la viongozi wawili wa soka kwenye Kamati ya Nidhamu kufuatia matukio ya utovu wa nidhamu yaliyojiri kwenye fainali hiyo.


Viongozi hao ni Jamal Salum Mohamed (Bui), pamoja na Ofisa kutoka klabu ya Simba, Ally Mohamed Shatry (Chico).

Hatua hii inakuja kufuatia kauli na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyofanywa na viongozi hao wakati na baada ya mchezo huo wa fainali ulioshuhudia mihemko na presha kubwa ya soka kisiwani Pemba.

Mara baada ya mchezo huo wa fainali, Bui alitoa tuhuma kuwa marefa wanaharibu mpira huku akitangaza kuwa yuko tayari timu hiyo ihamishiwe katika Ligi Kuu ya Zanzibar.

Hata hivyo haijulikani hasa, kosa la utovu wa nidhamu ambalo Chico amelifanya.

Kamati ya Mashindano imeamua ‘kuwaangushia rungu’ viongozi hao kwa kuwapeleka mbele ya vyombo vya maamuzi vya kisheria ili hatua kali zaidi za nidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi yao kulingana na kanuni za soka nchini.