Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEE WA FACT: Msimu ujao ligi iwe ya makundi kama ligi ndogo ya 2007



Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema ratiba ya msimu ujao itakuwa ngumu sana kwa vilabu shiriki vya ligi kuu ya NBC.

Akizungumza siku ya hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kigigitali wa kusimamia ligi, Karia alivitaka vilabu kuacha kulalamikia ugumu wa ratiba na badala yake vijikite katika kuandaa timu ikiwemo kusajili wachezaji wa kutosha.

"Tunawaomba kabisa; walimu, viongozi, wasemaji wa timu, waache zile habari za kwamba wachezaji wanachoka.

Na ndio maana tumetoa ruhusa ya kusajili wachezaji 40."

Karia akasisitiza kwamba uwepo wa matukio makubwa kama AFCON yamewalazimisha kupanga ratiba yenye mechi za karibu karibu ili msimu uishe mapema.


Ushauri wangu

Hii ni dharura ambayo hatuna hatuwezi kuikwepa.

Ni lazima tuhakikishe ligi inaisha mapema ili AFCON ambayo itafanyika nchini ikute msimu umeisha.

Kwa hiyo TFF na Bodi ya Ligi wangebadilisha muundo na mfumo wa ligi kwa msimu huu tu...kama dharura.

Hii ni kwa sababu huu ni msimu wa dharura, basi na tuishi kidharura.

Badala ya kucheza ligi ya kawaida ya nyumbani na ugenini, kuwe na ligi ya makundi itakayofanyika kwenye vituo.

Hii itarahisisha safari za timu na kuwafanya wachezaji kuweza kuhimili mechi za karibu karibu bila kukabiliana na uchovu wa safari ndefu.

Mfumo wa aina hii umeshatumika sana Tanzania....na ningependa kutolea mfano ulioofanyika mara mwisho.


Ligi ndogo 2007

Mwaka 2006 TFF chini ya Rais Leodger Chilla Tenga ilibadilisha mfumo wa ligi hapa nchini, kwa kufumua muundo na kalenda.

Mabadiliko haya yalikuja kuanza kutumika msimu wa 2007/08.


Muundo

Kabla ya mabadiliko haya kulikuwa na ligi TANO hapa nchini.

Ligi Kuu

Ligi daraja la kwanza

Ligi daraja la pili

Ligi daraja la tatu

Ligi daraja la nne.

Kupitia mabadiliko haya, ligi zote za chini ya ligi kuu zilifutwa, na kuanzishwa kwa ligi moja iliyoitwa ligi ya taifa.

Ligi ya taifa ilichezwa kuanzia ngazi ya wilaya na fainali zake za kitaifa zilifanyika kwenye vituo.

Kupitia ligi hii, timu ingeweza kuanzishwa msimu huu, na ikapanda hadi ligi kuu ndani ya msimu huu huu.

Azam FC ndio timu ya kwanza kufaidika na muundo huu mpya.

Wakati mabadiliko haya yanaanza kutumika msimu wa 2007/08, Azam FC ilikuwa daraja la tatu.

Kwa hiyo ikaangukia ligi ya taifa na ikafuzu kwa fainali zake katika kituo cha Dodoma... ikapanda.


Kalenda

Kalenda ya msimu wa wa soka Tanzania ulikuwa ukianza Februari na kumalizika Novemba.

Lakini mabadiliko yalifanya msimu mpya uanze Agosti na kumalizika Mei ya mwaka unaofuatia.

Kwa hiyo msimu mpya wa 2007/08 ulipangwa uanze Agosti 2007 na umakizike Mei 2008.

Lakini likaibuka tatizo moja. CAF bado ilikuwa inatumia kalenda ya kizamani ya Januari - Disemba.

Kwa hiyo mwaka 2008 mashindano ya Afrika yangeanza Februari 2008, ambapo ligi ya Tanzania ingekuwa haijaisha...na wawakilishi wake hawajapatikana.

Kwa hiyo ili kukabiliana na tatizo hili, TFF ikaandaa ligi ya dharura iliyoitwa ligi ndogo.

Ni ligi hii ndio ninayotaka TFF na Bodi ya Ligi wajifunze nayo.


Ilivyofanyika

Ligi hii ilifanyika mwaka 2007, kuanzia Aprili 14 hadi Julai 8.

Ilichezwa kwa makundi yaliyowekwa kwenye vituo....na iliendeshwa kwa awamu tatu.


Awamu ya kwanza - regular season

Kulikuwa na makundi matatu, na kila kundi likawekwa kwenye kituo chake.


Kundi A - kituo cha Arusha

Yanga

Polisi Morogoro

Moro United 6

Arusha FC

Kundi B - kituo cha Morogoro

Ashanti United SC

Simba SC

Prisons SC

Polisi Dodoma


Kundi C - kituo cha Dodoma

Mtibwa Sugar

JKT Ruvu Stars

Kagera Sugar

Ruvu Shooting Stars

Pan African


Timu za mbili za juu zilifuzu kwa AWAMU ya pili iliyoitwa SITA BORA, na zilizoshika mkia zilishuka daraja.

Awamu ya kwanza ilianza Aprili 14 na kuisha Mei 3.


Awamu ya pili - sita bora mtoano

Hii ilikuwa maalumu kwa ajili ya kutafuta bingwa na wawakilishi wa kimataifa.

Ilichezwa kwa makundi mawili ya kwenye vituo pia.


Kundi la Arusha

Yanga

JKT Ruvu Stars

Mtibwa Sugar


Kundi la Morogoro

Simba SC

Polisi Morogoro

Ashanti United

Kinara wa kila kundi alifuzu kwa fainali ambayo ilifanyika Julai 8 mjini Morogoro.


Awamu ya tatu - fainali

Hii ilikuwa fainali ambapo vinara wa makundi ya awamu walikutana.

Bingwa alipata tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa Afrika na aliyefungwa kwenye fainali alipata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho.

Yanga na Simba wakawa vinara wa makundi na wakacheza fainali hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Na baada ya mikwaju ya penati , Simba ikashinda kwa penati 4-3.

TFF ifanye hivyo

TFF na Bodi ya Ligi wanapaswa kurudi hadi 2007 kuchukua muundo wa ligi ile na kuitumia msimu ujao wa 2026/27.

Hii itasaidia sana kupunguza uchofu kwa wachezaji na kutunza nguvu kwenye AFCON.

Sisi timu yetu ya taifa inategemea wachezaji wanaocheza nyumbani, sio Ulaya kama wenzetu.

Tukiwachosha na ratiba ngumu, tunajikomoa wenyewe