Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa nidhamu mbovu, CAF yageuka mbogo AFCON

Muktasari:

  • Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zitafikia tamati huko Morocco, Januari 18, 2026.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeonyesha kukerwa na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyoonyeshwa katika mechi mbili za robo fainali ya AFCON 2025 zilizochezwa Ijumaa na Jumamosi huko Morocco.

Mechi hizo ni Morocco dhidi ya Cameroon iliyochezwa Ijumaa, Januari 9, 2026 na nyingine baina ya Nigeria na Algeria iliyochezwa, Jumamosi, Januari 10, 2026.

Taarifa iliyotolewa na CAF leo, Jumatatu, Januari 12, 2025 imeeleza kuwa Shirikisho hilo limeanzisha uchunguzi kwa baadhi ya matukio ya utovu wa nidhamu yaliyohusisha, wachezaji, maofisa wa timu na waandishi wa habari kwenye mechi hizo.

“CAF imekusanya ripoti za hivi karibuni za mechi pamoja na ushahidi wa video unaoonyesha kuwepo kwa vitendo vinavyoweza kuwa visivyokubalika vilivyofanywa na baadhi ya wachezaji na maofisa, na imefungua uchunguzi kuhusu matukio yaliyotokea wakati wa mechi za robo fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

“CAF imepeleka masuala hayo kwa Bodi ya Nidhamu kwa ajili ya uchunguzi na imesisitiza kuchukuliwa kwa hatua stahiki endapo watu waliotajwa watabainika kuwa na hatia ya ukiukwaji wowote.

“CAF pia inapitia picha za video za tukio linalohusisha wanahabari ambao inadaiwa walifanya vitendo visivyofaa katika eneo la mchanganyiko,” imefafanua taarifa hiyo ya CAF.

CAF pia imelaani vikali tabia zozote zisizofaa zilizojitokeza wakati wa mechi, hususan ile inayolenga waamuzi au waandaji wa mechi.

Kwa mujibu wa shirikisho hilo, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote ambaye mwenendo wake hauendani na maadili ya kitaaluma katika matukio ya CAF.

Katika mchezo baina ya Algeria na Nigeria, wachezaji wa timu hizo mbili mara kadhaa walionekana kuwa na mzozo na mwishoni mwa mchezo, baadhi ya maofisa na wachezaji wa Algeria waliwazonga waamuzi wa mchezo na kuonekana wakitaka kuwapiga, kwa kile kiachodaiwa kutoridhishwa na maamuzi ya mchezo huo ambao Nigeria ilishinda mabao 2-0.

Baada ya mchezo ambao Morocco ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cameroon, kumekuwa na shutuma nyingi zinazoelekezwa kwa marefa wa mchezo huo kwa madai ya kufanya maamuzi yaliyoonekana kuwapendelea Morocco.