Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Yanga awashtukia Waangola kwa Mkapa

FOLZ Pict

Kocha Mkuu wa Yanga, Romain Folz

Muktasari:

  • Yanga itashuka dimbani kesho dhidi ya Wiliete katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Romain Folz amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Wiliete akidai  atawashushia mziki kamili Waangola katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Kwa Mkapa, kesho.

Akizungumza leo, Folz amesema hana presha na lolote juu ya kikosi chake kwa kuwa kipo njia salama na kwamba timu  imeshinda mechi zote.

Amesema kutokana na ratiba ngumu ya mechi kuwa karibu mabadiliko ya timu yataendelea ili kuwajenga wachezaji.

Kocha huyo amethibitisha kwamba mchezo wa kesho atashusha kikosi kamili kitakachokwenda kutafuta ushindi licha ya kushinda mechi ya kwanza.

"Matokeo ya mchezo wa kwanza tumeshayaweka kando.  Nimewaambia wachezaji hii ni mechi tofauti na mpya tunatakiwa kutafuta ushindi mwingine ili tufuzu," amesema Folz.

"Kuhusu mabadiliko ya kikosi yataendelea. Narudia kwa hizi mechi zilizo karibu njia salama ni kuwapa nafasi wachezaji na kuwapumzisha wengine. Kila mchezaji aliye hapa (Yanga) ana kipaji kikubwa.

"Njia salama ni kuwapa nafasi ili waonyeshe (uwezo). Inawezekana baadhi yao kukatokea makosa hatua nzuri ni kujisahihisha.

"Kesho tutakuwa na timu kamili. Tutakuwa na mabadiliko. Tutakuwa na kikosi ambacho kitakwenda kuendeleza kasi yetu ya ushindi."