Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Yanga awazuia Mayele, Diarra

Muktasari:

  • Gamondi anayechukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyemaliza mkataba baada ya kuipa Yanga mataji saba tofauti ndani ya miaka miwili na nusu aliyokaa klabu hapo, anajiandaa kuja nchi ili kuanza  maandalizi ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya.

Mtaani kwa sasa mjadala ni kocha mpya wa Yanga, Miguel Angel Gamondi aliyetambulishwa juzi kwenye Mkutano Mkuu wa klabu hiyo, huku mwenyewe akiwa Latin Amerika ametuma salamu nzito akiwazuia nyota 11 wa kikosi cha sasa akiwamo Fiston Mayele na Diarra Djigui wasiondoke.

Gamondi anayechukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyemaliza mkataba baada ya kuipa Yanga mataji saba tofauti ndani ya miaka miwili na nusu aliyokaa klabu hapo, anajiandaa kuja nchi ili kuanza  maandalizi ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema mara baada ya kuanza mazungumzo na mabosi wa juu wa Yanga, akaingia kuanza kuangalia mechi kama tano  za kikosi zikiwamo tatu za Afrika na mbili za ligi kisha akanyanyua simu fasta kwa Rais Injinia Hersi Said.

Katika simu hiyo, kocha huyo raia wa Argentina aliyewahi kuzinoa timu kadhaa kubwa barani Afrika ikiwamo Mamelodi Sundowns, Wydad Casablanca na USM Alger, akataka mastaa wanaounda kikosi cha kwanza cha Yanga wasiopungua 10 wasiondoke hata mmoja wamsubiri.

Kocha huyo amewazuia wachezaji hao kwa kile kilichoelezwa kutotaka kuharibiwa mipango aliyonayo kwa msimu wake wa kwanza ndani ya timu hiyo iliyofika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kutetea Ngao ya Jamii pamoja na Makombe ya Ligi Kuu na ASFC.

Gamondi katika kupitia mechi hizo tano za Yanga, alijikuta akivutiwa na ubora na rekodi za mastaa wa kikosi cha kwanza akiwamo mfungaji bora wa ligi na Kombe la Shirikisho Afrika ambaye pia ndioye Mchezaji Bora wa msimu, Fiston Mayele sambamba na Stephane Aziz KI, Kennedy Musonda na kipa bora Djigui Diarra.

Kocha huyo aliyepewa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezwa atakapofanya vizuri, pia aliwazuia kuondoka viungo Khalid Aucho, winga Jesus Moloko, mabeki Dickson Job, Joyce Lomalisa, nahodha wao Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad 'Bacca' na Yannick Bangala.

Mbali na kuwazuia nyota hao 11, kocha huyo aliridhia kuondoka kwa mastaa wawili ambao ni mawinga Bernard Morrison na Tuisila Kisinda anayerejea klabu ya RS Berkane akiwaambia mabosi hao kwamba hakuna shida kupewa 'Thank You' kwa sababu zao za msingi.

Maelekezo hayo ya Gamondi, Mwanaspoti linafahamu kwa sasa mabosi wa Yanga watakuwa na kikao kizito kingine na Mayele kuhakikisha wanambakisha ili waende sawa na maelekezo ya kocha wao huyo.

Mayele baada ya kuwa na mafanikio katika miaka miwili amewapa ukweli mabosi wa Yanga kwamba anataka kutafuta changamoto mpya akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja.
Hata hivyo, mabosi wa Yanga kupitia tajiri wao Ghalib Said Mohamed 'GSM' hawataki kukubaliana na hilo haraka wakiona licha ya fedha nyingi ambazo wanaweza kuzipata hawataki kuibomoa timu yao kivile kwa kuamuachia Mkongomani huyo.

Yanga itakuwa na kazi rahisi kwa Lomalisa na Bangala ambao wameomba kuondoka klabuni hapo ambapo watasimamia mikataba yao au kuwabana kuzipeleka klabu wanazotaka kwenda ili wauzwe hatua ambayo wachezaji hao wameshindwa kuiweka wazi huku wakirejea makwao kwa mapumziko.