Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompyuta yaleta balaa zito EPL

KOMPYUTA Pict

Muktasari:

  • Kwenye uchambuzi huo wa kompyuta, Liverpool imepewa asilimia 28.5 ya kunyakua taji la Ligi Kuu England kwa mara ya pili mfululizo na itakuwa mara ya kwanza kwao kwenye historia ya ligi hiyo.

LONDON, ENGLAND: ACHANA na kilichotokea usiku wa jana Ijumaa, Liverpool imetabiriwa itatetea taji lake la Ligi Kuu England msimu huu, kwa mujibu wa uchambuzi wa kompyuta maalumu ya mtandao wa Opta.

Kwenye uchambuzi huo wa kompyuta, Liverpool imepewa asilimia 28.5 ya kunyakua taji la Ligi Kuu England kwa mara ya pili mfululizo na itakuwa mara ya kwanza kwao kwenye historia ya ligi hiyo.

Kikosi hicho cha Kocha Arne Slot kilibeba ubingwa wa ligi msimu uliopita bila ya kupewa changamoto yoyote na sasa inapambana kutetea taji hilo.

Arsenal imetajwa na kompyuta italeta ushindani kwenye mbio za ubingwa, lakini watakomea nafasi ya pili. Kompyuta imeipa Arsenal asilimia 24.3 na kushika namba mbili, huku Manchester City ikishika namba tatu. Kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola kimewekeza pesa nyingi kwenye usajili ili kubeba ubingwa, lakini kwa utabiri wa kompyuta ya Opta, miamba hiyo ya Etihad imepewa asilimia 18.8 na kushika namba tatu.

Manchester United yenye matumaini ya kufanya vizuri baada kikosi hicho cha Kocha Ruben Amorim kufanya vizuri kwenye pre-season kutokana na usajili wa Pauni 200 milioni, ikiwamo wa kumchukua straika Benjamin Sesko, hata hivyo, kompyuta ya Opta imetabiri itamaliza msimu nafasi ya 12, hata Top Six haimo. Itakuaje?

Kwenye upande mwingine wa msimamo wa ligi hiyo, Opta inatabiri Sunderland, Leeds United na Burnley zitashuka daraja kurudi kwenye Championship, huku jambo hilo litafanya kuwa msimu wa tatu mfululizo kwa timu zilizopanda daraja kushuka msimu huo huo.

Wolves imetabiriwa ni timu itakayoteseka sana msimu huu, lakini itamaliza nafasi ya 17. Hata hivyo, kompyuta imetabiri timu hiyo ina asilimia 7.3 ya kushuka daraja, ikidaiwa ni ndogo kulinganisha na Burnley (16.6), Leeds (17.8) na Sunderland (34.1).

Chelsea imetabiriwa ndiyo itakayokamilisha Top Four, huku kompyuta hiyo imeipa miamba hiyo ya Kocha Enzo Maresca asilimia 8.4 tu ya kuchukua ubingwa, jambo ambalo ni ndogo sana kwa kulinganisha na timu tatu za juu.

Wapinzani wao wa London, Tottenham, inayojiandaa kuwa na makali mapya chini ya Kocha Thomas Frank, imetabiriwa mabaya na kompyuta ya Opta kwa matokeo itamaliza kwenye nafasi ya 14 katika msimamo.

Licha ya kufanya mabadiliko makubwa ikiwamo kuuza mastaa wake mahiri, Brighton imetabiriwa itamaliza kwenye nafasi ya 10. Nottingham Forest ambayo ilishangaza wengi msimu uliopita, lakini Opta imedai msimu huu haitakuwa na makali kama yale, ilipokuwa ikishindania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya hadi siku ya mwisho ya msimu.

Crystal Palace imetabiriwa na kompyuta hiyo itamaliza nafasi ya saba, wakati Aston Villa na Newcastle zitabaki kwenye mchakamchaka wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya. Aston Villa ya kocha Unai Emery itamaliza nafasi ya tano na kurudi kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Newcastle ya Eddie Howe itamaliza namba sita.