Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lamine Yamal afikia thamani ya Sh992 bilioni

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa uchambuzi wa CIES, Yamal anaonekana kuwa “mchezaji wa kizazi kipya” ambaye thamani yake inaakisi sio tu uwezo wa sasa, bali pia mustakabali wake unaong’aa kwenye soka la dunia.

Barcelona, Hispania. Kwa mujibu wa tovuti ya takwimu za soka, CIES imebaini orodha ya wachezaji chipukizi wenye umri chini ya miaka 20 wenye thamani kubwa zaidi duniani na kinara wa orodha hiyo ni Lamine Yamal wa Barcelona, ambaye ametajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 308 (Sh992 bilioni).

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 amekuwa nyota wa dunia tangu msimu uliopita, akimaliza nafasi ya pili kwenye kuwania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu akiwa nyuma ya Ousmane Dembélé.

Mpaka sasa, Yamal amecheza mechi 116 akiwa na Barcelona, akifunga mabao 30 na kutoa pasi za mabao 40, sambamba na kushinda mataji mawili ya La Liga na Euro 2024 akiwa na timu ya taifa ya Hispania.

Msimu huu wa kiangazi, Yamal alisaini mkataba wa miaka sita na Barcelona ulioambatana na ongezeko kubwa la mshahara, hatua ambayo ilidhihirisha umuhimu wake kikosini.

Kwa mujibu wa CIES, thamani ya Yamal ni mara tatu zaidi ya anayemfuata, Estevão wa Chelsea, ambaye anatathminiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 104 (Sh335 bilioni).

Mbrazil huyo kijana mwenye umri wa miaka 18 amekuwa moto ndani ya klabu hiyo tangu kujiunga rasmi kutoka Palmeiras kwa ada ya pauni milioni 29, akifunga mabao manne katika mechi 15.

Wengine waliopo juu kwenye orodha hiyo ni Pau Cubarsí wa Barcelona mwenye thamani ya paundi milioni 99.2 (Sh320 bilioni), Franco Mastantuono wa Real Madrid paundi milioni 90 (Sh290 bilioni) na Warren Zaïre-Emery wa PSG paundi milioni 81.2 (Sh262 bilioni).

Vijana wa Arsenal watinga 10 bora

Arsenal imeweka vijana wawili kwenye orodha ya 10 bora, Ethan Nwaneri na Myles Lewis-Skelly, wote wamekulia kwenye akademi ya Hale End.

Nwaneri anatathminiwa kwa na thamani ya paundi milioni 78 (Sh251 bilioni), huku Lewis-Skelly akiwa na paundi milioni 75 (Sh241 bilioni).

Lewis-Skelly tayari amevunja rekodi kwa kuitwa timu ya taifa ya England na kucheza mechi sita, huku Nwaneri akitarajiwa kufuata nyayo zake baada ya kuisaidia England chini ya miaka 21 kubeba ubingwa wa Ulaya.

Chelsea na Spurs pia wamo

Mchezaji mwingine anayetarajiwa kujiunga na Chelsea msimu ujao, Geovany Quenda wa Sporting Lisbon, anatathminiwa kwa paundi milioni 71 (Sh229 bilioni) ikimaanisha Chelsea imepata dili zuri huku ikitarajiwa kuilipa klabu hiyo ya Ureno pauni milioni 40 (Sh130 bilioni).

Wengine waliokamilisha orodha ya 10 bora ni Endrick wa Real Madrid ambaye anathamani ya paundi milioni 64.4 (Sh208 bilioni) na Lucas Bergvall wa Tottenham (Sh193 bilioni), ambaye tayari amecheza mechi 60 tangu ajiunge kutoka Djurgården ya Sweden mwaka 2024.

Vipaji vingine vinavyopanda

Majina mengine yanayofuata kwenye orodha ya 20 bora ni pamoja na Jorrel Hato wa Chelsea, Archie Gray wa Tottenham, Leny Yoro wa Manchester United na Eli Junior Kroupi wa Bournemouth, ambaye amekuwa gumzo baada ya kufunga mabao manne katika mechi saba za Premier League.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa CIES, Yamal anaonekana kuwa “mchezaji wa kizazi kipya” ambaye thamani yake inaakisi sio tu uwezo wa sasa, bali pia mustakabali wake unaong’aa kwenye soka la dunia.

Thamani za wachezaji chipukizi 10 bora duniani

   Mchezaji              Klabu     Thamani kwa £  Thamani kwa Shilingi za Kitanzania 

1 Lamine Yamal    Barcelona £308m               ≈ Sh992 bilioni

2 Estevão                Chelsea £104m                  ≈ Sh335 bilioni

3 Pau Cubarsí        Barcelona £99.2m              ≈ Sh320 bilioni

4 Franco Mastantuono Real Madrid £90m     ≈ Sh290 bilioni

5 Warren Zaïre-Emery PSG £81.2m                  ≈ Sh262 bilioni

6 Ethan Nwaneri  Arsenal £77.5m                    ≈ Sh251 bilioni

7 Myles Lewis-Skelly Arsenal £74.6m             ≈ Sh241 bilioni

8 Geovany Quenda Sporting Lisbon £70.5m  ≈ Sh229 bilioni

9 Endrick Real Madrid £64.4m                           ≈ Sh208 bilioni

10 Lucas Bergvall Tottenham £60m                 ≈ Sh193 bilioni