Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Hispania yaanza na sare

Muktasari:

  • Msimu mpya wa La Liga umeanza huku timu zikiendelea kuonyeshana ubabe, Barcelona, Madrid kibarua kimeanza

Hispania. Ligi kuu nchini Hispania maarufu La Liga imeanza kutimua vumbi ambapo jana Agosti 15, 2024 ilichezwa michezo miwili ya ufunguzi  mchezo kati ya Athletic Club dhidi ya Getafe na mchezo mwingine ulikuwa kati ya Real Betis dhidi ya Girona, huku ikishuhudiwa michezo yote kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Ligi hiyo itaendelea tena leo Agosti 16 kwa michezo miwili ambapo klabu ya Celta Vigo watakuwa nyumbani kuwakaribisha Alaves saa 2:00 usiku, wakati Las Palmes watavaana na Sevilla saa 4:30 usiku.

Jumamosi itakuwa vuta ni kuvute nyingine ambapo klabu ya Barcelona watakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Valencia saa 4:30 usiku, Osasuna wao watakuwa nyumbani kuwakabili  Leganes ambao wamepanda daraja msimu huu wakitokea Segunda Division au “La Liga 2“ ambayo ndiyo Ligi ya pili kwa ukubwa ikitoka La Liga.

Mabingwa wa La Liga klabu ya Real Madrid watakuwa ugenini Jumapili saa 4:30 usiku dhidi ya klabu ya Mallorca. Msimu uliopita Real Madrid walitwaa taji la La Liga kwa jumla ya alama 95 ikiziaacha nyuma Barcelona, Girona, na Atletico Madrid.

Artem Dovbyk (27), nyota wa zamani wa Girona aliyetimkia AS Roma ya nchini Italia, ndiye aliyeshinda tuzo ya mfungaji bora wa La Liga msimu uliyopita wa 2023/2024 ambapo alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 24 akiwaacha nyuma Alexander Sorloth aliyekuwa na mabao 23 nyota wa zamani wa Villarreal aliyetimkia Atletico Madrid kwa Diego Simeone, pamoja na Jude Bellingham wa Madrid aliyefunga magoli 19 sawa na Robert Lewandowski wa Barcelona.

Msimu huu vita ya ubingwa pamoja na ile ya kuwania kiatu cha mfungaji bora inatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kwenye La Liga, kwani wameongezeka washambuliaji hatari kwenye ligi hiyo kama Kyllian Mbappe (25) aliyetokea klabu ya PSG na kujiunga na Real Madrid, pamoja na Julian Alvarez (24) aliyetokea Manchester City kwenda Atletico Madrid ambao wote ni wazuri kwenye kufumania nyavu.