Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maisha ya gerezani anayopitia Robinho

Muktasari:

  • Mahakama Kuu ya Brazil ilithibitisha hukumu hiyo mwaka 2022 na kumwamuru atumikie kifungo nchini humo.

São Paulo, Brazil. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Robson de Souza 'Robinho', anaendelea kutumikia kifungo kwenye moja ya gereza maarufu Brazili ambako alipelekwa baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji Italia mwaka 2017.

Robinho alihukumiwa kifungo cha miaka tisa gerezani Machi 2024 baada ya kupatikana na hatia hiyo ya ubakaji aliyotekeleza kwenye moja ya kumbi za starehe Italia, Januari 2013.

Mbrazili huyu ambaye aliwahi kuwa nyota wa Real Madrid na AC Milan, yupo kwenye gereza la Dr. Jose Augusto Cesar Salgado P2, Tremembe, lenye wafungwa wa matukio makubwa, akiwemo mwanamke aliyemuua binti yake mwenyewe mwaka 208, mwingine aliyefungwa miaka 98 kwa kumteka nyara na kumuua msichana wa miaka 15, pamoja na daktari aliyewadhulumu wagonjwa 39.

Mchezaji huyo alihukumiwa Italia mwaka 2017, lakini hakuweza kupelekwa huko kutokana na sheria za Brazil zinazopinga raia wake kusafirishwa kwa hukumu za nje. Hata hivyo, mwaka 2022 Mahakama Kuu ya Brazil ilithibitisha hukumu hiyo na kumweka nyota huyu gerezani nchini mwake.

Robinho anakumbana na maisha magumu gerezani, ambapo baadhi ya wafungwa wenzake waliruhusiwa kwenda likizo ya Krismasi na mwaka mpya, lakini yeye hakupata fursa hiyo huku familia yake ikilazimika kusherehekea sikukuu hizo bila yeye.

Kabla hajamaliza soka alicheza mechi 100 za kimataifa na kufunga mabao 28 akiwa na jezi ya Brazil. Katika klabu, alitamba sana akiwa na Real Madrid, Manchester City, na AC Milan kabla ya kurejea Santos kutokana na kashfa hiyo aliyoipata Italia.