Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford azitosa noti Uarabuni

Manchester, England. Marcus Rashford amekataa ofa tatu kutoka Saudi Arabia zinazofikia mshahara wa Pauni35 milioni kwa mwaka huku hatima yake ndani ya Manchester United ikiwa katika mabano.

Manchester United inajiandaa kumruhusu mshambuliaji huyo kuondoka katika dirisha hili la usajili la majira ya baridi baada ya mchezaji huyo kuwekwa kando na kocha mkuu wa timu hiyo, Ruben Amorim.

Na timu tatu tofauti za Saudi Arabia zimeonekana kuchangamkia fursa hiyo kila moja ikiripotiwa kutenga mshahara wa Pauni 35 milioni kwa mwezi, sawa na kitita cha Pauni 675,000 kwa wiki.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameonekana hayupo tayari kuchukua fungu hilo nono la mshahara kutoka Saudi Arabia na badala yake yuko tayari kupata mshahara pungufu wa huo aliondaliwa na timu za huko, ili abakie barani Ulaya.

Sababu kubwa ambayo inamfanya Rashford atamani kubakia katika mojawapo kati ya ligi za Ulaya ni kurudisha nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England, ambayo anaamini kwa kwenda Saudi Arabia atajiweka katika nafasi ngumu kuitwa na kocha na Thomas Tuchel kwa vile ligi hiyo haionekani kuwa ya ushindani.

Lakini sio tu ofa kutoka Saudi Arabia bali pia mshambuliaji huyo inaripotiwa kuwa hayupo tayari kwenda hata katika Ligi Kuu ya Uturuki.

Hofu ya kuendelea kwa kile kilichotokea kuanzia Aprili 2024 hadi sasa inaonekana ndio inachangia kumfanya Rashford aamue kutokwenda Saudi Arabia au Uturuki ikiwa mpango wa kuondoka Manchester United katika dirisha la usajili la majira ya baridi utakamilika.

Baada ya kujumuishwa katika kikosi cha England kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil, Machi mwaka jana, Rashford alishindwa kumshawishi aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate kumjumuisha katika fainali za Euro 2024 ambazo England ilipoteza katika fainali dhidi ya Hispania kwa kichapo cha mabao 2-1.

Lakini Rashford bado anaamini anayo fursa ya kurejea katika kikosi cha England kwa vile kwa sasa kinanolewa na kocha mpya, Thomas Tuchel lakini hili hilo litimie basi awe anacheza katika ligi kubwa Ulaya.

Inaripotiwa kuwa Manchester United itapokea na kusikiliza ofa zinazomuhusu mshambuliaji huyo katika dirisha linaloendelea la usajili ikiwa ni sehemu ya jitihada za klabu hiyo kuenda sawa na kanuni za mapato na matumizi na itakuwa tayari hata kumtoa kwa mkopo.

Rashford kwa sasa ni miongoni mwa nyota wanaolipwa kiasi kikubwa cha mshahara kwenye Ligi Kuu England ambapo kwa wiki anapokea kiasi cha Pauni 315,000.

Mchezaji huyo hajacheza mechi tano zilizopita za Manchester United ikiwemo dhidi ya Manchester City, mwezi uliopita.

Aliwekwa katika orodha ya wachezaji wa kutumika katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United, Jumatatu iliyopita lakini hakupewa nafasi ya kucheza huku timu yake ikichapwa mabao 2-0.

Inaripotiwa kwamba wachezaji wa Manchester United wamekuwa wakishangazwa na uamuzi huo wa kocha Amorim kumuondoa kikosini kwa vile mshambuliaji huyo na kiungo Bruno Fernandes ndio wafungaji wao bora kwenye ligi hadi sasa ambapo kila mmoja amefunga mabao manne.

Rashford alianza kuchezea kikosi cha wakubwa cha Man United mwaka 2015.