Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makambo aachana na Horoya

Muktasari:

Makambo alisaini mkataba wa miaka mitatu na Horoya akitokea Yanga, lakini hajawa na wakati mzuri na mabosi hao wa Guinea.

MSHAMBULIAJI Heritier Makambo ameachana na klabu yake ya Horoya inayoshiriki Ligi Kuu nchini Guinea baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufanyika.

Makambo alisajiliwa na Horoya kwa mkataba wa miaka mitatu na mpaka sasa alikuwa ameitumikia timu hiyo kwa misimu miwili tu.

Kuvunjwa kwa mkataba huo ni taarifa nzuri kwa mabosi wa Yanga ambao inaelezwa wamekuwa wanahitaji mchezaji huyo arejee katika kikosi chao.

Ilielezwa Yanga walipeleka ombi la kuhitaji kumsajili mchezaji huyo lakini ilishindikana kutokana na mabosi wa Horoya kuhitaji pesa nyingi.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram ya klabu ya Horoya ulimshukuru Makambo kwa kuwa nae kwa misimu miwili mfululizo na kumtakia kila la kheri.

“Ahsante (Mercì) kwa misimu miwili tangu ulivyofika, tunakutakia kila la kheri katika kipaji chako,” ilieleza taarifa hiyo.