Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matano ushindi wa Arsenal dhidi ya Milan

Muktasari:

  • Arsenal wanatarajia kuvaana na Newcastle kwenye mchezo ujao katika ziara hiyo.

Singapore. Arsenal imeanza vyema maandalizi ya msimu mpya baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya AC Milan kwenye Uwanja wa Taifa wa Singapore, bao pekee likifungwa na Bukayo Saka kipindi cha pili.

Lakini mbali na matokeo, hizi hapa pointi tano kubwa tulizojifunza kutoka kwenye mchezo huo wa kirafiki:

1. Ethan Nwaneri amerudi upya

Chipukizi wa miaka 18, Ethan Nwaneri, ameonesha kiwango cha juu kiasi kwamba kocha wa England, Thomas Tuchel, ana kila sababu ya kumchukua Kombe la Dunia lijalo (2026) litakalofanyika Marekani, Kanada na Mexico.

Akiwa kwenye nafasi ya namba 10, alileta usumbufu mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya Milan. Mbinu zake, kasi, na uthubutu wake wa kuingia kwenye boksi ni vitu vilivyomtofautisha.

2. Max Dowman ameandika historia

Katika dakika za mwisho, jina lingine liliibuka Max Dowman. Akiwa na miaka 15 tu, kijana huyo aliingia na kuonyesha jeuri isiyo ya kawaida. Kuingia kwake sekunde 60 tu baadaye alitengeneza nafasi na kujaribu kupiga shuti.

Muonekano wake, utulivu na uchezaji wake unaonesha si wa kawaida kwa umri wake. Kama ataendelea hivi, jina lake litasikika tena.

3. Mrithi wa Saliba apatikana

Wakati wengi wakitafuta beki wa kati wa siku zijazo, Arsenal tayari wana Marli Salmon, kijana mwingine wa miaka 15 ambaye alionekana imara na jasiri. Pasi yake ya mita 60 hadi kwa Reiss Nelson ilikumbusha uchezaji wa William Saliba.

Beki mwenzake upande wa kulia, Josh Nichols (18), naye alionyesha kiwango cha kipekee licha ya kuwa mdogo kiumri. Hakika, hazina ya vipaji ndani ya Arsenal ni pana kuliko inavyoonekana.

4. Kai Havertz bado hajathibitisha thamani yake

Licha ya kupewa nafasi kama mshambuliaji wa kati, Kai Havertz alishindwa kuonesha makali yanayohitajika. Japokuwa alionekana kuongezeka kimwili, bado hana uthubutu wa kushambulia lango moja kwa moja.

Kwa ujio wa Viktor Gyokeres kutoka Sporting, presha juu ya Havertz sasa ni kubwa. Ana kazi ya ziada kuonyesha kuwa anastahili kuwa chaguo la kwanza.

5.Tiketi ghali, mashabiki wachache

Katika uwanja unaobeba zaidi ya mashabiki 55,000, waliokuwepo walikuwa 22,813 tu pungufu ya nusu. Licha ya mechi kuwa na burudani ya kutosha, bei ya tiketi kuanzia pauni 70 (Sh 244,767) ilionekana kuwa kikwazo kikubwa.

Iwapo Arsenal wanataka kukuza soko la Asia, watahitaji mikakati ya kuvutia mashabiki ikiwemo kupunguza gharama kwa mechi za kirafiki kama hizi.

Arsenal wanatarajia kuvaana na Newcastle kwenye mchezo ujao katika ziara hiyo.