Man United kwa PSG, Liverpool kwa Bayern hapatoshi
Muktasari:
- Real Madrid ndiyo timu pekee iliyoweka rekodi katika karne hii kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mara tatu mfululizo
London, England. Manchester United na Liverpool zitakuwa na kibarua kizito katika Ligi ya Mabingwa baada ya kupangwa na Paris St-Germain na Bayern Munich katika mechi za ratiba ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.
Mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City na Tottenham watacheza dhidi ya miamba ya Bundesliga. City itawavaa Schalke huku Spurs watakuwa na kibarua kwa Borussia Dortmund.
Mechi za kwanza za raundi 16 bora zitachezwa kati ya Februari 12, 13, 19 na 20, wakati mechi za marudiano zitakuwa Machi 5, 6, 12 na 13.
Vinara wa Makundi watacheza mechi ya kwanza ugenini na marudiano watakuwa nyumbani.
Mabingwa watetezi Real Madrid pamoja na kuwa na msimu mbaya bado wamepata ratiba nyepesi kidogo baada ya kupagwa na Ajax.
Barcelona wenyewe watakuwa ugenini dhidi ya Lyon, wakati Atletico Madrid watamkaribisha Ronaldo na Juventus. Roma watakuwa wenyeji wa Porto.
Ratiba ya Ligi ya Mabingwa
Schalke vs Manchester City
Atletico Madrid vs Juventus
Manchester United vs Paris Saint-Germain
Tottenham vs Borussia Dortmund
Lyon vs Barcelona
Roma vs Porto
Ajax vs Real Madrid
Liverpool vs Bayern Munich