Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United mzuka mwingi dili la Mbeumo

Muktasari:

  • Mchezaji ambaye Brentford inamtaka aje kurithi mikoba ya Mbeumo ni staa wa Ipswich Town, Omari Hutchinson kama mtu sahihi kwenye mpango wao huo na imeanza kuulizia namna ya kumpata.

London, England. Brentford imeshampata mchezaji ambaye inamtazama kuwa mwafaka wa kuja kuchukua mikoba ya Bryan Mbeumo, ambaye anahusishwa na mpango wa kutua Manchester United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Mbeumo, 25, amekuwa kwenye rada za Man United kwenye dirisha hili wakati kocha wa miamba hiyo ya Old Trafford, Ruben Amorim akihitaji kuboresha safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.

Kwa mujibu wa gwiji wa masuala ya usajili na uhamisho wa wachezaji, Fabrizio Romano, Man United imepata nguvu kubwa kwenye mpango wao wa kumnasa staa huyo wa kimataifa wa Cameroon baada ya kuona timu yake ya Brentford kuanza mchakato wa kupata mbadala wake.

Mchezaji ambaye Brentford inamtaka aje kurithi mikoba ya Mbeumo ni staa wa Ipswich Town, Omari Hutchinson kama mtu sahihi kwenye mpango wao huo na imeanza kuulizia namna ya kumpata.

Ipswich imeshashuka daraja ipo kwenye Championship, hivyo Brentford inaamini inaweza kumpata mkali huyo, ambaye msimu uliopita alionyesha kiwango bora licha ya timu yake kushuka daraja.

Hivyo, Brentford inapambana kumrudisha kwenye Ligi Kuu England mchezaji, Hutchinson, ambaye aliwahi kuichezea Chelsea. Na wakifanikiwa kwenye hilo, huenda ikamruhusu Mbeumo kwenda Man United baada ya kugomea ofa mbili za klabu hiyo ya Old Trafford.

Mkurugenzi wa soka wa Brentford, Phil Giles alisema Mbeumo anaweza kubaki kwenye kikosi chao endapo kama Man United itashindwa kufikia malipo ya Pauni 65 milioni ambayo wanataka ilipwe.

Giles alisema: “Kama ataondoka basi kwa vigezo vyetu. Mabao 20 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita kutoka kwa Mbeumo, tulitarajia timu nyingi kumtaka. Kama ataondoka kwa sasa, basi jambo hilo litakuwa limetupatia pesa za kutosha, hilo tumeliweka wazi.”


MECHI TISA ZA KWANZA ZA MAN UTD EPL

Agosti 17 vs Arsenal (nyumbani)

Agosti 23 vs Fulham (ugenini)

Agosti 30 vs Burnley (nyumbani)

Septemba 13 vs Man City (ugenini)

Septemba 20 vs Chelsea (nyumbani)

Septemba 27 vs Brentford (ugenini)

Oktoba 4 vs Sunderland (nyumbani)

Oktoba 18 vs Liverpool (ugenini)

Oktoba 25 vs Brentford (nyumbani)