Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United wamuweka Tavernier kwenye rada

Mshambuliaji wa Bournemouth, Marcus Tavernier. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • United pia wanatarajia kusajili viungo wawili wapya pamoja na kuimarisha nafasi za mabeki wa pembeni na beki wa kati.

Manchester, England. Manchester United imeongeza jina la mshambuliaji wa Bournemouth, Marcus Tavernier, kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa kusajiliwa katika dirisha la usajili la majira ya joto.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya kocha wa muda wa United, Michael Carrick, kuthibitisha kuwa klabu hiyo inapanga kuimarisha nafasi ya winga wa kushoto.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu, maskauti wa United wanaendelea kuchunguza chaguo mbalimbali, huku majina mengine yakitajwa katika orodha hiyo yakijumuisha Morgan Gibbs-White wa Nottingham Forest pamoja na winga wa RB Leipzig, Yan Diomande.


Ushindani uko hapa

Tavernier pia anatajwa kuwaniwa na klabu ya Aston Villa pamoja na Nottingham Forest, ambao waliwahi kuonesha nia ya kumsajili mwezi Januari kabla ya mchezaji huyo kupata majeraha ya msuli wa paja.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 19, aliyekulia katika akademi ya Middlesbrough, amekuwa mhimili muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Bournemouth.

Msimu huu amefunga mabao sita na kutoa pasi tano za mabao licha ya kukumbwa na majeraha.


Bournemouth kusikiliza ofa

Inaelezwa kuwa Bournemouth wanaweza kuwa tayari kumuuza mchezaji huyo ikiwa watapokea ofa nzuri, kwani klabu hiyo imekuwa ikifanya biashara ya kuuza na kununua wachezaji ili kupata faida na kuwekeza katika vipaji vipya.

Tavernier ana mkataba unaodumu hadi mwaka 2029 na thamani yake inaweza kufikia hadi pauni 40 milioni.


Mpango wa usajili United

Hata hivyo, mpango wa mwisho wa usajili wa United utategemea nafasi watakayomaliza msimu huu. Kufuzu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kunaweza kuwapa uwezo mkubwa wa kuvutia wachezaji wakubwa.

Mbali na winga, United pia wanatarajia kusajili viungo wawili wapya pamoja na kuimarisha nafasi za mabeki wa pembeni na beki wa kati.

Wakati huohuo, aliyekuwa mkuu wa mafunzo na maendeleo ya wachezaji katika Klabu ya Manchester City, Darren Hughes, anatarajiwa kujiunga na akademi ya Manchester United kama mkuu wa maendeleo ya soka la vijana.