Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yagonga mwamba kwa Martinez

Muktasari:

  • chaguo lingine ni kipa chipukizi wa Royal Antwerp, Senne Lammens, ingawa bado maamuzi ya mwisho hayajafikiwa.

Jaribio la Manchester United kumsajili kwa mkopo kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez, limegonga mwamba hatua inayowaacha wakihaha kuziba pengo golini baada ya Andre Onana kuumia na kukosa baadhi ya mechi za mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu England.

Kocha wa United, Ruben Amorim, tayari amefanikisha usajili wa washambuliaji wawili Matheus Cunha kutoka Wolves na Bryan Mbeumo kutoka Brentford lakini sasa anahangaika kutafuta mtu wa kuimarisha safu ya ulinzi nyuma kabisa ya kikosi chake.

Amorim alimtaja Martinez, bingwa wa dunia na timu ya taifa ya Argentina, kuwa chaguo lake kuu la kukamilisha mabadiliko ya kikosi katika dirisha hili la usajili. Hata hivyo, jaribio la kumchukua kwa mkopo lilikataliwa vikali na Aston Villa mwishoni mwa wiki.

Taarifa zinaeleza kuwa United walifanya mazungumzo ya awali ya chini chini kuhusu uwezekano wa kumsajili Martinez kwa mkopo, lakini maofisa wa Villa walipokea wazo hilo kwa mshangao mkubwa na kulikataa papo hapo.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye alitimuliwa kwa kadi nyekundu katika mechi ya mwisho ya msimu uliopita dhidi ya Man United, alisaini mkataba wa muda mrefu na Aston Villa mwaka jana unaomfunga hadi 2029 jambo linalofanya uwezekano wa kuondoka kwake kuwa mdogo mno.

Villa wameweka thamani ya Martinez kuwa si chini ya pauni milioni 40, na haijulikani kama United wako tayari kufikia kiwango hicho kwa sasa.

Wakati hali ya Onana ikiendelea kuwa ya sintofahamu kufuatia jeraha la msuli wa paja, United wanaendelea kufikiria mbadala huku chaguo lingine ni kipa chipukizi wa Royal Antwerp, Senne Lammens, ingawa bado maamuzi ya mwisho hayajafikiwa.

United bado hawajatoa taarifa rasmi kuhusu sakata hilo, huku Aston Villa wakisisitiza hawajapokea mawasiliano yoyote ya moja kwa moja kutoka Old Trafford.

Hali hii inaweka presha kubwa kwa Amorim, ambaye anataka kikosi chake kipate muundo kamili mapema kabla ya kuanza kwa msimu mpya.