Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yaondolewa kwa fedheha Kombe la Carabao

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza kabisa United inafungwa na timu ya Daraja la Nne katika historia ya mashindano ya vikombe vya ndani.

Manchester United imejikuta ikiondoshwa kwa fedheha kubwa kwenye Kombe la Carabao baada ya kutolewa kwa penalti na Grimsby Town, timu ya Daraja la Nne ya England, yakiwa ni matokeo ya aibu zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Blundell Park ilishuhudiwa United ikiondolewa kwa penalti 12-11 baada ya sare ya mabao 2-2 baada ya dakika 90 na zile za ziada kutamatika. Hii ni mara ya kwanza United inafungwa na timu ya Daraja la Nne katika historia ya mashindano ya vikombe vya ndani.

Kocha Ruben Amorim, aliyekuja Old Trafford kwa matumaini makubwa baada ya kupewa fedha nyingi kwenye usajili wa kiangazi, hali sasa inazidi kuwa mbaya. Timu yake tayari ilikuwa imeshindwa kupata ushindi kwenye michezo miwili ya kwanza ya Ligi Kuu na sasa inakumbwa na kipigo cha aibu.

Onana matatani tena

Kipa Andre Onana, ambaye amekuwa akikosolewa tangu msimu uliopita, tena alijikuta lawamani. Bao la kwanza la Grimsby lilipatikana dakika ya 15 kupitia Charles Vernam aliyepiga shuti kali na kumwacha Onana akitazama mpira ukitinga wavuni. Kabla ya hapo, kipa huyo alionekana kusuasua akiokoa mpira wa kichwa kutoka kwa Cameron Gardner.

Dakika chache baadaye, Grimsby waliongeza bao la pili kwa urahisi. Onana alitoka golini kujaribu kuudaka mpira wa krosi lakini akashindwa kuugusa sawasawa, na kumpa Tyrell Warren nafasi ya kupachika mpira wavuni bila kizuizi.

Mashabiki wa Grimsby walishindwa kujizuia, nyimbo za “sacked in the morning” zilimiminika zikimlenga Amorim ambaye alionekana kupoteza mwelekeo kwenye eneo la benchi.

Mabadiliko ya pili hayakutosha

United walijaribu kurejea mchezoni kipindi cha pili baada ya Amorim kuwaleta Bruno Fernandes, Matthijs de Ligt na Mbeumo ili kuongeza nguvu. Ingawa walionekana bora zaidi, bado walishindwa kuibadili Grimsby ambayo ilicheza kwa nidhamu.

Bryan Mbeumo alipunguza bao kwa shuti kali dakika ya 72, kabla ya Harry Maguire kuunganisha kona ya Mason Mount dakika ya 89 na kusababisha mchezo kuingia muda wa nyongeza na baadaye penalti.


Mikwaju ya penalti

Kila mchezaji alionekana kuwa na presha. Onana alidhani ameiokoa United baada ya kuzuia penalti ya Clarke Oduor, lakini makosa ya nyota wapya yalikuja kuliangusha tena klabu hiyo.

Matheus Cunha alipiga mkwaju uliokolewa na kipa wa Grimsby. Hatimaye, Bryan Mbeumo alipiga penalti ikagonga mwamba na kurudi nje na hapo ndipo ukawa mwisho wa safari ya Man United kwenye Kombe la Carabao msimu huu.

Sesko, aliyesajiliwa kwa dau kubwa kutoka RB Leipzig, bado hajatokea kuwa mkombozi. Hata kwenye penalti, alijitokeza kucheza miongoni mwa waliokuwa wa mwisho jambo lililoibua maswali kuhusu ujasiri wake.

Kwa upande wa Onana, makosa yanaweza kuchochea uongozi wa United kuharakisha mpango wa kumsajili kipa mpya, baada ya tetesi za kuhusishwa na Senne Lammens wa Royal Antwerp.