Manula 'out' Simba, Kakolanya aanza!

WAWAKILISHI wa michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba, muda mfupi baadaye watacheza na Al Merrikh ya Sudan huku kipa wao Aishi Manula akiukosa mchezo huo.

Simba wanacheza mechi ya tatu ya makundi ya ligi hiyo baada ya kushinda mbili za mwanzo dhidi ya As Vita bao 1-0 na Al Ahly bao 1-0, mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni mjini Khartom.

Muda mchache kuanzia sasa kikosi hicho kitawekwa hadharani na kitakuwa na mabadiliko machache ambapo nafasi ya Manula itachukuliwa na Beno Kakolanya.

Kakolanya ndio ataanza langoni huku kwenye benchi atakuwepo Ally Salim kwani Manula ameokena kutokuwa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya

Mabeki wa pembeniĀ  watakuwa ni Shomary Kapombe,l na Mohammed Hussein 'Tshabalala.

Mabeki wa kati wataanza Pascal Wawa na Joash Onyango kama ilivyokuwa katika mechi mbili za mwanzo.

Eneo la kiungo wakabaji ataanza Taddeo Lwanga, Mzamiru Yassin.

Viungo washambuluaji ni Rally Bwalya, Clatous Chama na Luis Miquissone wakati straika ataanza Chriss Mugalu.