Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa yaziwahi Simba na Yanga utambulisho

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa na Mashujaa FC jana imesema kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mchezo utakahusisha kikosi cha wanawake cha timu hiyo 'Mashujaa Queens'.

Dar es Salaam.  Mashujaa FC imepanga kuanika hadharani nyota wake itakaowatumia msimu huu wa 2025/2026 Jumapili wiki hii, Septemba 7 mwaka huu katika Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Zoezi hilo la utambulisho ambalo litafanyika siku hiyo ya kilele cha tamasha la Klbu hiyo lijulikanalo kama 'Mashujaa Day' litaenda sambamba na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu kutoka nje ya nchi ambayo wataitangaza hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa na Mashujaa FC jana imesema kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mchezo utakahusisha kikosi cha wanawake cha timu hiyo 'Mashujaa Queens'.

"Siku ya Watanganyika ni 07.09.2025. Hii ni tofauti na zote unazozifahamu kwani utashuhudia maajabu haya, Vazi la kifahari kuzinduliwa, Mashujaa Queens kurejea nyumbani, kuwashuhudia wachezaji bora zaidi wa kizawa, mchezo mkubwa wa kimataifa na burudani za kutosha," imefafanua taarifa hiyo ya Mashujaa FC.

Hii ni mara ya tatu kwa Mashujaa FC kufanya Tamasha la Mashujaa ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2023 ambapo katika siku ya kilele cha tamasha hilo ilicheza na timu ya Inter Stars kutoka Burundi.

Katika kujiandaa na msimu ujao, Mashujaa FC inaendelea na kambi yake ya maandalizi ambayo imeiweka Dar es Salaam kama ilivyo kwa kikosi cha Mashujaa Queens.

Baadhi ya nyota ambao watatambulishwa katika tamasha la Mashujaa Day ni Samson Madeleke, Sele Bwenzi, Salum Kihimbwa, Samwel Onditi, Hamad Kabasele, Sued Juma, Mudathir Said na Omary Omary.

Msimu uliopita, Mashujaa FC ilimaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 35 ambazo ilizivuna baada ya kuibuka na ushindi katika mechi nane na kutoka sare 11 huku ikipoteza mechi 11.