Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Ghana kuoga mamilioni kufuzu Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Timu 13 tofauti za Taifa barani Afrika zimewahi kushiriki Fainali za Kombe la Dunia kwa nyakati tofauti ambazo ni Ghana, Cameroon, Misri, Afrika Kusini, DR Congo, Tunisia, Morocco, Algeria, Togo, Angola, Nigeria, Senegal na Ivory Coast. 

Nyota wa timu ya Taifa ya Ghana 'Black Stars' kila mmoja atapata kitita cha Dola 5,000 (Sh12 milioni) kama bonasi ya ushindi wa mchezo wa jana dhidi ya Comoro ambao umeifanya ijihakikishie tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitafanyika Marekani, Canada na Mexico mwakani.

Bao pekee la Mohammed Kudus katika dakika ya 47 akimalizia pasi ya Thomas Partey limetosha kuifanya Ghana kufikisha pointi 25 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote kwenye Kundi I la mashindano ya kuwania kufuzu Fainali hizo kupitia bara la Afrika na hivyo kuipa uhakika wa kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya tano.

Na nyota walioshiriki kuipeperusha vyema bendera ya Ghana jana, hawajaondoka mikono mitupu kwani kila mmoja amepata kiasi hicho cha fedha ambacho serikali ya Ghana inatoa kama bonasi ya ushindi kwa mechi ambayo timu hiyo inashinda katika mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Wakati wachezaji kila mmoja akipata Dola 5,000, Kocha Mkuu wa Black Stars, Otto Addo yeye pekee amepata kitita cha Dola 10,000 (Sh25 milioni).

Mbali na fedha ambazo wamepata kwa bonasi, wachezaji wa Ghana na maofisa wa benchi la ufundi pia watagawana kiasi cha Dola 27,000 (Sh55 milioni) kama posho ya siku kwa muda wa siku nane ambazo wamekuwa kambini kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Comoro.

Ghana imekuwa timu ya taifa ya tano barani Afrika kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 ikifuata nyayo za Morocco, Tunisia, Misri na Algeria.

Hii itakuwa ni mara ya tano kwa Ghana kushiriki Fainali za Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo katika Fainali za 2006, 2010, 2014 na 2022.

Kama atakuwepo katika Fainali za mwakani, nahodha wa Ghana, Jordan Ayew atafikia rekodi ya kucheza fainali za mashindano hayo kwa mara tatu ambazo ni nyingi zaidi akifuata nyayo za Andre Ayew, Sulley Muntari na Asamoah Gyan.

Kocha Mkuu wa Ghana, Otto Addo ataingia katika historia ya kuwa miongoni mwa makocha wachache duniani ambao wamewahi kushiriki Kombe la Dunia wakiwa wachezaji na kisha wakiwa makocha.