Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa sita waibua presha Arsenal, kocha afichua siri

Muktasari:

  • Arsenal inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) ikiwa na pointi 70 ilizokusanya katika mechi 31.

Wachezaji sita wa Arsenal wamejitoa katika vikosi vya timu zao za taifa vilivyoitwa hivi karibuni, jambo linaloweza kuibua wasiwasi kwa timu hiyo inapokaribia mechi za mwishoni mwa msimu.

Gabriel Magalhaes amekuwa mchezaji wa sita katika orodha hiyo baada ya kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil.

Wachezaji wengine ni William Saliba, Leandro Trossard, Jurrien Timber, Martin Odegaard na Eberechi Eze.

“Vipimo vya picha vimethibitisha kwamba Gabriel Magalhaes hayuko fiti kucheza kwenye mechi katika kipindi hiki cha mapumziko ya kimataifa ya FIFA.

“Hakuna mchezaji ambaye ataitwa kuchukua nafasi yake,” taarifa ya Timu ya Taifa ya Brazil imethibitisha.

Hata hivyo Meneja wa timu ya Taifa ya Norway, Stale Solbakken amefichua siri kuwa Odegaard ameachwa kwa sababu ya tahadhari tu.

“Kitu cha muhimu ni kwamba yuko amejiandaa vilivyo kwa ajili ya majira ya kiangazi.

“Na itakuwa kituko kulazimisha kitu kwamba ambacho hatudhani kwamba ni busarakwa sababu tu atakuwepo,” amesema Solbakken.

Kibarua kinachofuata kwa Arsenal ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Southampton, Aprili 4, 2026.

Siku tatu baadaye itakabiliana na Sporting Lisbon katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.