Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe kiboko akipiga ‘hat trick’ ya Ufungaji Bora

Muktasari:

  • Mbappe ndio Mfungaji Bora wa muda wote wa Fainali za Kombe la Dunia akiwa na mabao 22.

Kylian Mbappe amemaliza Fainali za Kombe la Dunia 2026 akiwa na rekodi tatu ambazo zinaweza kuchukua muda mrefu kuvunjwa na wachezaji wengine.

Kwanza ameweka rekodi ya kuwa Mfungaji Bora wa muda wote wa Fainali za Kombe la Dunia akiwa na mabao 22.

Nyota na nahodha huyo wa Ufaransa amefanya hivyo kwa kuvunja rekodi ya Lionel Messi aliyekuwa na mabao 21.

Mbappe pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuwahi kuwa Mfungaji Bora wa Kombe la Dunia katika matoleo mawili tofauti tena mfululizo.

Mbappe alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia 2022 akiwa na mabao nane na katika fainali za mwaka huu amemaliza akiwa na mabao 10.

Rekodi ya tatu ambayo ni ya kibabe zaidi ambayo Mbappe ameiweka ni kuwa mchezaji pekee duniani kushinda tuzo ya Mfungaji Bora katika mashindano matatu makubwa tofauti ndani ya msimu mmoja.

Ukiondoa ufungaji bora wa Kombe la Dunia, Mbappe amekuwa pia mfungaji bora wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ akiwa na mabao 25 na pia amekuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga mabao 15.