Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Olise avunja rekodi ya miaka 56 Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Pelé alitoa pasi sita za mabao katika michezo sita wakati Brazil ilipotwaa Kombe la Dunia mwaka 1970.

Rekodi ya gwiji wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento 'Pele' iliyodumu kwa miaka 56 katika fainali za Kombe la Dunia, imevunjwa rasmi na winga wa Ufaransa, Michael Olise usiku wa kuamkia leo kwa muda wa Afrika Mashariki katika mechi ya kuwania mshindi wa tatu wa Kombe la Dunia baina ya Ufaransa na Hispania.

Pasi mbili za mabao ambazo Olise alipiga katika mchezo huo, zimemfanya nyota huyo awe mchezaji aliyetoa pasi nyingi za mwisho katika toleo moja la Kombe la Dunia, akimaliza na idadi ya pasi saba.

Katika mechi hiyo, Ufaransa ilipoteza kwa mabao 6-4. Pelé alitoa pasi sita za mabao katika michezo sita wakati Brazil ilipotwaa Kombe la Dunia mwaka 1970.

Hilo lilikuwa Kombe la Dunia la mwisho kwa Pelé, na pia lilikuwa taji la tatu la Brazil katika mashindano hayo akiwa sehemu ya kikosi.

Kwa kuwa Kombe la Dunia la mwaka huu lina idadi kubwa zaidi ya timu ambazo ni 48, Olise alicheza mchezo mmoja zaidi kuliko Pelé, ingawa yeye pia alifikia wastani wa pasi moja ya bao kwa kila mchezo.

Olise aliingia kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu siku ya Jumamosi akiwa tayari ametoa pasi tano za mabao, kisha akatoa pasi mbili zilizosababisha mabao yote mawili ya Mbappé.

Pasi iliyomfikisha kusawazisha rekodi ya Pelé ilitolewa katika dakika ya 48, wakati Ufaransa ilipoanza kupunguza pengo la mabao baada ya kuwa nyuma kwa mabao 4-0 dhidi ya England mwishoni mwa kipindi cha kwanza.