Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeumo atumika dili la Baleba kutua Man United

Muktasari:

  • Kiungo wa Brighton, Baleba aliivutia Man United na kupelekewa ofa kadhaa kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini klabu yake iligoma kumpiga bei.

YAOUNDE, CAMEROON. Staa wa Manchester United, Bryan Mbeumo ameripotiwa kumhamasisha mchezaji mwenzake wa Cameroon, Carlos Baleba waungane pamoja Old Trafford.

Kiungo wa Brighton, Baleba aliivutia Man United na kupelekewa ofa kadhaa kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini klabu yake iligoma kumpiga bei.

Man United bado inahitaji huduma ya Baleba na inaweza kufanya jaribio jingine la kutaka saini yake wakati dirisha la Januari litakapofunguliwa.

Kinachoelezwa kwa sasa ni kwamba Mbeumo anafanya kazi ya kumshawishi Baleba wakati walipokutana kwenye timu ya taifa Cameroon.

Mbeumo ana miezi michache tu huko Old Trafford, lakini anaamini Man United ni mahali salama kwa mchezaji mwenzake huyo kwenda kucheza soka lake.