Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbosso kukiwasha Simba Day, awapa ahadi mashabiki

Muktasari:

  • Tamasha la Simba Day hufanyika kila mwaka likitumiwa na klabu ya Simba kutambulisha kikosi chake.

Msanii wa Bongo Fleva Mbosso amethibitisha kutumbuiza kwenye kilele cha tamasha kubwa la klabu ya Simba 'Simba Day' Septemba 10, 2025  katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba imeweka wazi leo kupitia msemaji wake Ahmed Ally ambapo Mbosso atakuwa jukwaani kuwapa burudani mashabiki wa klabu hiyo.

Meneja Msaidizi wa Habari wa Klabu ya Simba, Ally Shatry 'Chico' amesema lengo la kumchagua Mbosso katika Tamasha la msimu huu kwa sababu ni msanii anayefanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya bongo fleva.

Amesema Chico, kuhusu kuwaacha wasanii wengine wakubwa akiwemo Ali Kiba, Chico amesema Ali Kiba ndiye msanii pekee aliyetumbuiza miaka miwili mfululizo kama msanii rasmi mwaka 2023 na 2024.

"Kila mwaka huwa tunaalika msanii rasmi na wasanii wengine kutumbuiza kwenye tamasha msanii huyo anakuwa ni yule ambaye yuko kwenye 'peak' na anayependwa na watu. Hivyo mwaka huu uongozi umeona Mbosso apewe hiyo nafasi na wasanii wengine wataendelea kutajwa," amesema Chico.

Kwa upande wake Mbosso amesema kuwa kutokana na mapenzi yake makubwa kwa klabu ya Simba na ukizingatia yeye ni mshabiki wa Simba kindakindaki, hivyo ameushukuru uongozi wa Simba kwa kumpa fursa ambapo amewahakikishia kutoa burudani nzuri.

"Najua watu wengi wanafahamu mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, nimekuwa nikitumia talanta yangu katika sanaa ya muziki, hivyo nimeamua kutoa 'surprise' kwenye tukio la  Simba Day kwa ajili ya mashabiki wa Simba," amesema Mbosso.

Aidha Mwananchi Digital ilimuuliza Mbosso kama atatunga wimbo maalumu wa Simba ama atatumia kutumbuiza nyimbo zake hasa wimbo wa 'Pawa' ambao ameuachia hivi karibuni na kupata umaarufu kwa mashabiki zake ambapo ametoa ufafanuzi juu ya hilo.

"Hii sasa ya kutunga wimbo maalumu wa Simba ama kutumia nyimbo zangu za Bongofleva, hii ni siri yangu ila kikubwa niwaombe  mashabiki wa Simba Septemba 10 wafike kwa wingi kwa ajili ya kushuhudia burudani nitakayoitoa," amesema Mbosso

Mbosso kwa sasa anavuma na Albamu yake inayoitwa  Room Namba  3  yenye nyimbo   Pawa, Nusu saa, Aviola,  Tena, Siko Single, Athuman, Merijah .