Micho ahukumiwa kifungo miaka mitatu Sauzi

Thursday October 21 2021
MICHOPIC
By Mwandishi Wetu

CAPE TOWN, AFRIKA KUSINI. MAHAKAMA ya Afrika Kusini imemhukumu kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin “Micho” Sredojevic kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na makossa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia, alisema mwendesha mashtaka juzi Jumanne.

Micho aliripotiwa kufanya kosa hilo mwaka jana wakati alipokuwa akiinoa Zambia.

“Mapema asubuhi (juzi Jumanne), mahakama ya Port Elizabeth ilimkuta na hatia kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, Milutin Sredojevic, katika makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia,” ilifichua taarifa ya Mamlaka ya Taifa ya Mashtaka (NPA).

Hukumu ya kifungo cha miaka mitatu inaweza kugeuka na kuwa cha miaka mitano kama atafanya kosa jingine la aina hiyo.

Tukio hilo lilitokea Desemba 2020 katika michuano iliyofanyika katika mji wa Gqeberha, Afrika Kusini ambao zamani ulifahamika kama Port Elizabeth.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 39 alikuwa akifanya kazi ya kugawa kahawa uwanjani hapo, ndipo alipomuuliza Micho kama atahitaji sukari kwenye kahawa yake, ambapo Mserbia huyo alisema “hapana na kisha kuongeza kwamba anataka sukari ya aina nyingine, akionyesha kidole kwenye sehemu za siri za mwanamke huyo,” ilibainisha NPA.

Advertisement

Baadaye siku hiyo hiyo, alipoletewa kahawa “Sredojevic alimshika maeneo yake ya siri “.

Advertisement