Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshangao kwa vigogo, Kombe la Dunia likiwa mlangoni

Muktasari:

  • Mechi ya ufunguzi wa Fainali za Kombe la Dunia imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Azteca, Mexico City, kuanzia saa 4:00 usiku baina ya wenyeji Mexico na Afrika Kusini.

Baadhi ya mechi za kimataifa za kirafiki zilizochezwa jana katika nchi tofautio, zimeibua mshtuko kwa baadhi ya timu za taifa zinazopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu huko Marekani, Canada na Mexico.

Matokeo ya kupoteza au sare dhidi ya timu ambazo zinaonekana kama sio tishio kwao, yanaonekana kama kengele ya hatari kwa mabenchi ya ufundi ya timu hizo, yakihitajika kurekebisha udhaifu ulioonekana kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Mchezo ambao umekuwa na matokeo ya kushangaza ni ule uliochezwa katika Uwanja wa Municipal de Riazor jijini La Coruna ambao wenyeji Hispania wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Iraq.

Ferran Torres alitangulia kuifungia bao Hispania katika dakika ya 16 na Iraq walisawazisha katika dakika ya 27 kupitia kwa Merchas Doski.

Ni matokeo ambayo yameonekana kumshtua Kocha Mkuu wa Hispania, Luis De La Fuente ambaye amesema Iraq imeonyesha kiwango ambacho hawakukitegemea na pia kimewaonyesha yale yanayotakiwa kufanyiwa kazi.

"Wametushangaza sana katika mtazamo chanya. Tumepata wakati mgumu katika kipindi cha kwanza kuzuia ujenzi wa mashambulizi yao. Kila mechi ni ngumu, lakini walionyesha kasi ya mchezo, nguvu kubwa, na ushirikiano mzuri katika kupiga pasi. Ni timu ya kuvutia yenye nguvu na ari kubwa. Walitusukuma hadi mwisho na kufanya mambo kuwa magumu kwetu," amesema De la Fuente.

Matokeo mengine ya kushtua ni kuichapo cha mabao 2-1 ambacho Ufaransa imekipata ikiwa nyumbani kutoka kwa Ivory Coast.

Licha ya kutangulia kufunga bao katika dakika ya 45 kupitia kwa Rayan Cherki, Ufaransa ilijikuta ikiruhusu mabao mawili ya Ivory Coast katika kipindi cha pili yaliyofungwa na Guela Doue na Amad Diallo.

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps amewataka wachezaji wake kuyachukulia matokeo hayo kama angalizo kwao kuelekea katika Kombe la Dunia.

"Matokeo ya kupoteza hayavutii hata kama tulifanya baadhi ya vitu vizuri katika kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili tulifanya mabadiliko mengi lakini huo sio utetezi. 

"Hatukuwa wazuri kama tulivyokuwa kabla ya mapumziko, na wao walileta kasi kubwa ya mchezo.Tunakabiliwa na timu ya aina hiyo hiyo tarehe 16 Juni," amesema Deschamps.


Matokeo ya mechi za kirafiki kwa timu zinazoshiriki Kombe la Dunia

Hispania 1-1 Iraq

Ufaransa 1-2 Ivory Coast

Panama 4-2 Jamhuri ya Dominika

Korea Kusini 1-0 El Salvador

Sweden 2-2 Ugiriki