Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshery rasmi Yanga, aanza matizi Avic

KIPA namba moja wa Mtibwa Sugar, Aboutwaleeb Mshery (21) leo Desemba 29 amemalizana na vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Mshery amejiunga na Yanga, tayari kwa ajili ya kuziba pengo la kipa namba moja wa timu hiyo Djigui Diarra ambaye ameenda Mali kwenye majukumu ya timu ya taifa wanaojiandaa na michuano ya Afcon.

Kipa huyo tayari amewasili kambi ya Yanga, iliyopo Avic Town Kigamboni, ambako alitambulishwa mbele ya wachezaji wenzake, wakati wa mazoezi, kisha akarudi kwenye gari alilokuja nalo.

Baadae Mshery alibadilisha nguo na kuvaa jezi na kwenda kujiunga na wenzake mazoezini katika programu ya kocha Nabi.

Kipa huyo tayali amepewa jezi namba 50 mgongoni na kupewa glavu tayari kwa ajili ya mazoezi.

Yanga wameanza mazoezi ya kuelekezwa kwa kutumia ubao wakiwa wamekaa chini na kocha Nabi akiwa anawaelekeza kwa kuandika.