Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mudathir bado yupo sana Yanga aongeza miwili

Muktasari:

  • Mudathir Yahya alijiunga na Yanga, Januari 2023 akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Azam FC.

Dar es Salaam. Kiungo Mudathir Yahya ataendelea kuitumikia Yanga kwa miaka miwili baada ya kusaini mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo.

Mkataba wa awali wa miaka miwili na nusu baina ya kiungo huyo na Yanga ulifikia tamati mwishoni mwa msimu uliomalizika na hivyo alikuwa huru kujiunga na timu nyingine.

Hata hivyo Yanga imeonesha nia ya kuendelea naye na leo imetangaza rasmi kuwa nyota huyo kutoka Visiwani Zanzibar ataendelea kuwepo kikosini.

“Simu ziendelee kuita, Mudathir Yahya bado yupo sana Jangwani,” imesema sehemu ya taarifa ya Yanga.

Tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2023, Mudathir Yahya ameonyesha uwezo mkubwa katika safu ya kiungo huku pia akiwa tishio mara kwa mara anaposogea mbele kusaidia mashambulizi.

Mbali na uwezo wa kuzuia na kuchezesha timu, Mudathir poa ameonyesha uwezo wa kufumania nyavu mara kadhaa anapopata nafasi akiwa jirani na eneo la hatari la timu pinzani.

Uthibitisho wa hilo ni msimu wa 2023/2024 ambao alikuwa mfungaji bora namba mbili wa Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo alifumania nyavu mara tisa.