Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika huyu ni chaguo la kocha Yanga

Muktasari:

  • Hatua hiyo inakwenda kufifisha zaidi hesabu za Yanga kumsajili mshambuliaji Jonathan Sowah wa Singida Black Stars, aliyekuwa anapigiwa hesabu awali.

Kabla hata hajatambulishwa wala kugusa Uwanja wa mazoezi, anayedaiwa kuwa kocha wa Yanga Romain Folz ametoa maagizo mazito ya kutaka asajiliwe mshambuliaji Andy Boyeli.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga, ni kwamba Folz ambaye inaelezwa tayari yupo nchini, ametaka aletewe mshambuliaji huyo wa Shekhukhune  United ya Afrika Kusini.

Boyeli ambaye ni raia wa DR Congo ndio chaguo la kocha huyo akisema hana mashaka juu ya ubora wa mshambuliaji huyo.

Hata hivyo, mabosi wa Yanga wameshindwa kukubaliana na bei ya mshambuliaji huyo wakitaka kwanza kumpata kwa mkopo staa huyo ambaye amewahi kucheza Power Dynamos ya Zambia.

Boyeli sio jina geni kwa mabosi wa Yanga kwani aliwahi kuingia kwenye hesabu zao mwaka 2023, alipokuja nchini akiifunga Simba

wakati wa mchezo wa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi iliyopigwa Oktoba Mosi pale Azam Complex, Chamazi.

Mshambuliaji huyo aliwafunga Simba dakika ya 17 lakini akiangulia kuwapa ugumu mabeki wa wenyeji wao, kwenye mechi hiyo iliyomaizika kwa sare ya bao 1-1, wekundu hao bao lao likisawazishwa na aliyekuwa mshambuliaji wao John Bocco dakika ya 69.

Yanga italipa kiasi cha dola 20,000 kwenye mkataba huo wa mkopo lakini kama itakubali uwezo wake italazimika kutumia kiasi cha dola 100,000.

Boyeli ni mshambuliaji anayejua kufunga lakini akiwa na nguvu za kupambana na mabeki akiwa na uwezo wa kuutunza mpira katikati ya mabeki.

Hatua hiyo inakwenda kufifisha zaidi hesabu za Yanga kumsajili mshambuliaji Jonathan Sowah wa Singida Black Stars, aliyekuwa anapigiwa hesabu awali.

Staa huyo msimu uliopita alifanikiwa kuichezea timu yake mechi 25 kwenye PSL na kufunga mabao sita, bado ana mkataba na timu yake hadi 2027.