Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzimu wa Dabi unavyoendelea kumtafuna Fadlu Morocco

Kocha wa Raja Athletic, Fadlu Davis. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Fadlu ameendelea kuteseka na mechi za dabi kwani hata wakati alipokuwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba hakuweza kutamba dhidi ya Yanga.

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa kocha wa Simba, Fadlu Davis ambaye kwa sasa anainoa Raja Casablaca ya Morocco, ameendelea kupata wakati mgumu katika mechi za watani wa jadi ‘dabi’ baada ya jana Mei 9, 2026 kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzani wao Wydad Athletic Club katika dabi ya Casablanca.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Morocco ‘Botola Pro’, wenyeji Raja Casablanca walikubali kipigo hicho ambacho kimeifanya timu hiyo kushindwa kuongeza tofauti ya pointi dhidi ya wapinzani wao wa karibu Maghreb Fez na FAR Rabat ambao wana faida ya mechi moja mkononi kwa kila timu.

Raja Casablaca wanaongoza msimamo wa ligi kwa pointi 39 wakifuatiwa na Maghreb Fez wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 38 wakati FAR Rabat nao wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 37 na iwapo timu hizo zikiibuka na ushindi katika mechi zao za leo basi Raja Casablanca wataporomoka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Tangu alipotua Raja Casablanca, Septemba mwaka jana hii ilikuwa mechi ya pili ya dabi hiyo kwa kocha Fadlu ambapo mechi ya kwanza ilichezwa Oktoba 29, 2025 na kuisha kwa suluhu.

Fadlu ameendelea kuteseka na mechi za dabi kwani hata wakati alipokuwa na Wekundu wa Msimbazi, Simba kocha huyo hakuweza kutamba katika pambano la Watani wa Jadi dhidi ya Yanga ‘Kariakoo Derby’ ambapo alipoteza mechi zote nne.

Katika mechi hizo nne, mbili zilikuwa za Ngao ya Jamii na mbili zilikuwa za Ligi Kuu Bara.

Fadlu raia wa Afrika Kusini ana kibarua kigumu cha kuirudisha Raja Casablanca kwenye kilele cha ligi zikiwa zimebaki mechi 10 kutamatika.