Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Núñez kumpisha mshambuliaji mpya Liverpool

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Núñez ameendelea kuhusishwa na klabu ya Napoli ya Italia pia timu tajiri ya Al-Hilal kutoka Saudi Arabia.

Klabu ya Liverpool imeweka wazi kuwa kusajili mshambuliaji wa kiwango cha juu ni kipaumbele chao kikubwa katika dirisha hili la usajili, huku mazungumzo ya kuuzwa kwa Darwin Núñez yakitarajiwa kuharakishwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Athletic, Núñez (26) ameendelea kuhusishwa na klabu ya Napoli ya Italia na pia timu tajiri ya Al-Hilal kutoka Saudi Arabia. Hata hivyo, dili na Napoli linaonekana kuwa gumu kutokana na Liverpool kutaka dau la takribani pauni milioni 70 (Sh213 bilioni).

New Content Item (1)

Liverpool waanza kusaka mrithi wake

Katika mipango ya kuimarisha safu ya ushambuliaji, Liverpool wameweka majina kama Alexander Isak wa Newcastle na Hugo Ekitike wa Eintracht Frankfurt kama chaguo kuu.

Kwa mshangao pia, Nicolas Jackson wa Chelsea ametajwa kuwa mmoja wa wachezaji walioko kwenye rada ya Liverpool. Ripoti zinaeleza kuwa mkurugenzi mpya wa michezo wa Liverpool, Richard Hughes, alikuwa shabiki wa Jackson alipokuwa Bournemouth. Hata hivyo, uwezekano wa kumnasa kwa sasa ni mkubwa kwani Chelsea wametangaza kumpiga bei kwenye dirisha hili lausajili.

Wengine waliokuwa kwenye orodha ya awali ya Liverpool ni pamoja na Viktor Gyökeres ambaye yupo karibu kujiunga na Arsenal licha ya vikwazo kadhaa kuwepo, Victor Osimhen ambaye anatajwa kuwa mbioni kusalia moja kwa moja Galatasaray baada ya mkopo wake kutoka Napol kumalizika na João Pedro ambaye tayari amesaini na Chelsea kwa pauni milioni 60.

New Content Item (1)

Mauzo huenda yakatoa nafasi kwa usajili mpya

Hadi sasa, Liverpool wameshatumia takribani pauni milioni 185 (Sh610 bilioni) kwa usajili wa wachezaji wanne ambao ni Florian Wirtz, Jeremie Frimpong, Giorgi Mamardashvili pamoja na Milos Kerkez.

Kutokana na matumizi hayo makubwa, mauzo ya baadhi ya wachezaji yanahitajika ili kufanikisha usajili mwingine. Miongoni mwa waliowekwa kwenye orodha ya kuuzwa ni Darwin Núñez, ambaye anaonekana kama mchezaji wa kwanza kuondoka.

Kwa mujibu wa Corriere dello Sport, rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis ndiye anashughulikia moja kwa moja mazungumzo ya kumsajili Núñez, kupitia wakala Fali Ramadani. Ikiwa Napoli watakataa dau la Núñez, kuna uwezekano wakageukia Lorenzo Lucca wa Udinese, ambaye anagharimu karibu pauni milioni 34 (Sh112 bilioni).

New Content Item (1)

Kifo cha Diogo Jota chabadilisha hesabu

Kifo cha ghafla cha mshambuliaji Diogo Jota kimebadili kabisa hesabu za Liverpool. Mreno huyo alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Arne Slot msimu uliopita na ingawa alihusishwa na kuondoka, alikuwa anatarajiwa kuwa mhimili msimu huu.

Kwa sasa, upungufu katika safu ya ushambuliaji unafanya Liverpool kuzidi kuharakisha kusajili mshambuliaji namba tisa mpya kabla ya msimu mpya kuanza.