Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndege ya Ronaldo yaondoka Saudi Arabia

Muktasari:

  • Ndege hiyo imepitia anga la Misri na Bahari ya Mediterania kabla ya kutua Hispania.

Riyadh, Saudi Arabia. Ndege binafsi inayomilikiwa na nyota wa soka wa Ureno, Cristiano Ronaldo, imeruka kutoka Saudi Arabia usiku wa manane kuelekea Madrid, Hispania, hatua inayozua maswali iwapo mshambuliaji huyo ameondoka nchini humo kufuatia kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi Mashariki ya Kati.

Ronaldo (41), ambaye anaishi Riyadh pamoja na mpenzi wake Georgina Rodriguez na watoto wao watano, yupo Saudi Arabia tangu alipojiunga na klabu ya Al-Nassr.

Taarifa zinasema jiji la Riyadh limekumbwa na mashambulizi ya anga huku ubalozi wa Marekani ukidaiwa kulengwa na ndege zisizo na rubani. Mashambulizi hayo ni sehemu ya mvutano unaoendelea kati ya Israel, Marekani dhidi ya Iran.

Ndege binafsi ya mshambuliaji wa Ureno na Al-Nassr, Cristiano Roanldo ambaye bado hajajulikana kama ameondoka Saudi Arabia baada ya kuibuka kwa machafuko huko Mashariki ya kati. Picha na Mtandao


Ndege yaruka usiku wa manane

Kwa mujibu wa taarifa za ufuatiliaji wa safari za ndege, ndege aina ya Bombardier Global Express 6500 inayomilikiwa na Ronaldo imeondoka Riyadh saa 8:00 usiku na kuwasili Madrid saa 1:00 asubuhi. Ndege hiyo imepitia anga la Misri na Bahari ya Mediterania kabla ya kutua Hispania.

Tukio hilo limekuja wakati raia wa kigeni wakiripotiwa kuondoka kwa wingi katika mataifa ya Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea.

Ronaldo alinunua ndege hiyo mwaka 2024 kwa thamani ya pauni 61 milioni (Sh180 bilioni), baada ya kuuza ndege yake ya awali aina ya Gulfstream G200.

Mpenzi wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez, akiwa ndani ya  ndege hiyo. Picha na Mtadao

Ndege hiyo ya rangi nyeusi ina uwezo wa kubeba hadi abiria 15 na ina vyumba vya kifahari, ikiwamo sehemu ya mapumziko, kitanda cha watu wawili na bafu maalumu. Pia imepambwa kwa nembo yake binafsi na picha ya umbo lake akishangilia bao.

Mbali na hali ya usalama, Ronaldo pia kwa sasa anakabiliwa na majeraha ya misuli aliyoyapata katika ushindi wa mabao 3-1 wa Al-Nassr dhidi ya Al-Fayha mwishoni mwa wiki.

Mshambuliaji huyo, anayelipwa Sh1.7 bilioni kwa siku katika Ligi Kuu ya Saudi, alilazimika kutolewa uwanjani na sasa anasubiri matokeo ya vipimo vya kitabibu, huku Kombe la Dunia likikaribia.

Mashambulizi ya pamoja ya Israel na Marekani dhidi ya Iran yameripotiwa kusababisha vifo vya viongozi wa ngazi za juu. Picha na Mtandao

Wakati huohuo, mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Asia kati ya Al-Nassr na Al-Wasl imeahirishwa kutokana na hali ya usalama katika ukanda huo.

Mashambulizi ya pamoja ya Israel na Marekani dhidi ya Iran yameripotiwa kusababisha vifo vya viongozi wa ngazi za juu, huku Iran ikijibu mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Ronaldo au wawakilishi wake kuthibitisha iwapo safari ya ndege hiyo inahusiana moja kwa moja na hali ya usalama, lakini tukio hilo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka duniani.