Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nuno atimuliwa Forest, bosi atajwa

Muktasari:

  • Makocha wengine wanaohusishwa na kibarua hicho cha kwenda kuinoa Nottingham Forest ni Ange Postecoglou na Jose Mourinho, ambao kwa sasa hawana kazi yoyote.

London, England. Kocha Nuno Espirito Santo amefutwa kazi kwenye kikosi cha Nottingham Forest.

Mmiliki wa klabu hiyo, Evangelos Marinakis ameamua kumpiga chini kocha huyo baada ya wawili hao kuwa na uhusiano mbaya kwa muda sasa.

Hata hivyo, tajiri Marinakis baadaye alidai amekuwa na uhusiano mzuri na kocha huyo licha ya kuwapo na sitomfahamu baina ya Nuno na bosi wa usajili, Edu aliyejiunga na timu hiyo akitokea Arsenal.

Lakini, baada ya kipigo cha mabao 3-0 nyumbani kutoka kwa West Ham United kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa jambo hilo limemfanya tajiri huyo kumfuta kazi Nuno.

Taarifa fupi ya klabu hiyo ilisomeka: "Nottingham Forest Football Club inathibitisha kutokana na hali iliyopo, Nuno Espírito Santo amekubali kuachana na wajibu wake wa kuwa kocha mkuu. Klabu inamshukuru Nuno kwa mchango wake katika kipindi cha mafanikio hapa The City Ground, hasa kwa msimu wa 2024/25 ambao utamfanya akumbukwe daima kwenye historia ya klabu.

"Mtu ambaye alikuwa na umuhimu mkubwa msimu uliopita kwenye mafanikio yetu, tutamkumbuka daima na atakuwa spesho katika safari yetu."

Nuno, 51, alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kubaki City Ground, Juni 21 mwaka huu. Lakini, mwezi mmoja baadaye kulianza kuibuka ripoti uhusiano wake na mwenye timu, Marinakis umekuwa kwenye mashaka makubwa.

Sasa kocha wa Celtic, aliyewahi kuinoa Liverpool, Brendan Rodgers anahusishwa na kibarua hicho cha kwenda kurithi mikoba ya Nuno. Tajiri Marinakis ameripotiwa kuwa shabiki mkubwa wa kocha huyo wa zamani wa Leicester City.

Makocha wengine wanaohusishwa na kibarua hicho cha kwenda kuinoa Nottingham Forest ni Ange Postecoglou na Jose Mourinho, ambao kwa sasa hawana kazi yoyote.