Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyakati za mwisho Ligi Kuu Bara

Muktasari:

  • Metacha Mnata wa Singida Black Stars ambaye anaonekana kupoteza nafasi mbele ya Amas Obasogie, anazo clean sheet saba ambapo mara ya mwisho aliipata Desemba 16, 2024 dhidi ya Tanzania Prisons.

Keshokutwa Jumatano, Ligi Kuu Bara inaendelea kwa mzunguko wa 29, kisha Jumapili ijayo kwa maana ya Juni 22, zitachezwa mechi za mzunguko wa 30. Baada ya hapo, zitafahamika timu zitakazocheza mtoano kuwania kubaki ligi kuu kwa msimu ujao. Hiyo ni kutokana na zile mbili KenGold na Kagera Sugar kushuka moja kwa moja mapema.

Wakati hayo yakifahamika, itasubiriwa mechi ya wakongwe, Yanga na Simba ikiwa ni Dabi ya Kariakoo iliyosogezwa hadi Juni 25 kutoka Juni 15, hii ndiyo itafunga msimu wa Ligi Kuu Bara 2024-2025.

Ligi hiyo iliyosimama kwa muda, inaendelea huku kukiwa na vita nyingi zinakwenda kushindaniwa. Kuna wanaowania ubingwa, hapa inaihusu Yanga inayoongoza msimamo na pointi 73 na Simba yenye 72. Timu hizo mbili ndizo zina nafasi kwa mojawapo kubeba ubingwa zikiwa tayari zimekata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Azam iliyopo nafasi ya tatu na Singida Black Stars ya nne, nazo zinataka heshima tu kumaliza juu ya mwenzake, lakini hata kama zikiteleza, haziwezi kutoka nafasi nne za juu. Kumbuka tayari zina tiketi ya msimu ujao kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Ukiachana na vita iliyopo kwa kila timu ikipambana kumaliza nafasi nzuri kwenye msimamo zikifahamu kwamba kuna fungu la fedha kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo upande wa haki za matangazo, kuna wachezaji wanasaka heshima kutokana na rekodi kuwakataa kwa muda. Nyota hao katika mechi zilizosalia, wanaweza kuzitumia vizuri kumaliza msimu kwa heshima.


WASHAMBULIAJI

Kwa sasa kuna vita ya kuwania ufungaji bora ambapo kinara ni Jean Charles Ahoua wa Simba mwenye mabao 15, anafuatia Clement Mzize (13) na Prince Dube (13) wanaocheza Yanga.

Lakini katika eneo la ushambuliaji, kuna wachezaji wamekuwa na ukame wa mabao licha ya awali kuonyesha kiwango bora.

Pale Kagera Sugar kuna Peter Lwasa mwenye mabao manane, mara ya mwisho alifunga Machi 7, 2025 dhidi ya Pamba Jiji, amekaa takribani miezi mitatu bila ya kutikisa nyavu.

Heritier Makambo wa Tabora United, naye mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa Februari 14, 2025 dhidi ya KenGold, kwa sasa ana mabao matano.

Kennedy Musonda wa Yanga mwenye mabao matatu, mara ya mwisho alifunga Februari 1, 2025 dhidi ya Kagera Sugar huku Crispin Ngushi wa Mashujaa aliyepachika mabao mawili, naye mara ya mwisho alifunga Desemba 28, 2024 dhidi ya Dodoma Jiji.

Wengine ni Maabad Maulid (Coastal Union mabao 5), mara ya mwisho alifunga Februari 7, 2025 dhidi ya JKT Tanzania. Zidane Sereri wa Azam, wakati yupo Dodoma Jiji alifunga mabao matatu, akatua Azam akafunga mabao mawili jumla yakawa matano. Mara ya mwisho alifunga Februari 24, 2025 dhidi ya Simba.

Mishamo Michael wa KenGold tangu alipofunga Machi 5, 2025 dhidi ya Mashujaa, hajafunga tena akibaki na mabao matano sawa na Oscar Paul wa KMC ambaye naye mara ya mwisho alifunga Machi 6, 2025 dhidi ya Fountain Gate.

Mkongwe John Bocco wa JKT Tanzania ambapo taarifa zinasema ataagwa rasmi Juni 22 kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Mashujaa, ana mabao mawili ambayo yote aliyafunga Oktoba 18, 2024 dhidi ya Tabora United.


VIUNGO

Licha ya kwamba kazi ya kwanza ya kiungo mshambuliaji ni kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji, lakini nao wamekuwa wakitikisa nyavu inapobidi. Mfano mzuri ni Jean Charles Ahoua wa Simba anayeongoza chati ya ufungaji na mabao 15.

Ukija kwa viungo wengine ambao walianza vizuri na sasa kama wamepunguzwa makali ni Offen Chikola wa Tabora United mwenye mabao saba ambaye mara ya mwisho alifunga Machi 7, 2025 dhidi ya JKT Tanzania.

Selemani Bwenzi wa KenGold mwenye mabao matano ambayo yote ameyafunga mwezi Februari, tangu hapo hajacheka na nyavu. Hana tofauti na Marouf Tchakei wa Singida Black Stars ambaye naye mara ya mwisho alifunga Februari 7, 2025 dhidi ya Kagera Sugar. Kwa sasa ana mabao matano.

Kinara wa asisti, Feisal Salum wa Azam FC mwenye nazo 13, amefunga mabao manne pekee, kumbuka msimu uliopita alikuwa nyuma ya kinara wa ufungaji Aziz KI ambapo Fei Toto alifunga mabao 19. Aziz KI akimaliza na 21. Kiungo huyo tangu umeingia mwaka 2025, hajafunga bao, mara ya mwisho alifunga Desemba 1, 2024 dhidi ya Dodoma Jiji.

Elie Mpanzu wa Simba, aliwaka sana Februari na Machi alipofunga mabao matatu, kumbuka alitua Simba kipindi cha dirisha dogo, hadi sasa hajafunga bao, kutokana na kuendelea kupata nafasi ya kucheza, anayo nafasi ya kumaliza msimu kwa kutikisa nyavu. Mara ya mwisho alifunga Machi 14, 2025 dhidi ya Dodoma Jiji.

Wengine baadhi ni Salum Kihimbwa (Fountain Gate, mabao manne, mara ya mwisho alifunga Desemba 25, 2024 dhidi ya Namungo), Awesu Awesu (Simba, mabao mawili, mara ya mwisho alifunga Novemba 6, 2024 dhidi ya KMC) na Kibu Denis (Simba mabao mawili, yote alifunga Machi 14, 2025 dhidi ya Dodoma Jiji).


MAKIPA

Kipengele hiki ni kuhusu clean sheet, ukiangalia kule juu, Moussa Camara wa Simba anaongoza akiwa nazo 17 akifuatiwa na Djigui Diarra wa Yanga mwenye 15. Kuna makipa wengine wanapata nafasi kubwa ya kucheza, lakini suala la kuondoka na clean sheet kipengele.

Kipa namba moja wa JKT Tanzania, Yacoub Suleiman Ali aliye na clean sheet nane, huu ni mwezi wa nne sasa hajafanikiwa kuipata ya tisa, mara ya mwisho kutoka uwanjani bila ya kuruhusu bao ilikuwa Februari 21, 2025 dhidi ya Kagera Sugar.

Metacha Mnata wa Singida Black Stars ambaye anaonekana kupoteza nafasi mbele ya Amas Obasogie, anazo clean sheet saba ambapo mara ya mwisho aliipata Desemba 16, 2024 dhidi ya Tanzania Prisons.

Pia kuna Chuma Ramadhani (Coastal Union, clean sheet sita huku ya mwisho akiipata Februari 23, 2025 dhidi ya Namungo FC), Jonathan Nahimana (Namungo, clean sheet tano, ya mwisho aliipata Februari 23, 2025 dhidi ya Coastal Union) na Ramadhan Chalamanda (Kagera Sugar, clean sheet tano, ya mwisho aliipata Februari 26, 2025 dhidi ya KMC).