Nyota VPL watawala kikosi cha Stars

Sunday June 13 2021
stars pic
By Ramadhan Elias

ZIKIWA zimesalia dakika chache kuanza kwa mechi ya kirafiki kati ya Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Malawi, tayari kikosi cha Stars kinachoanza kimewekwa wazi.

Kwenye mchezo huo ambao upo kwenye kalenda la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Polsen amewapa nafasi wachezaji 10 wanaocheza ligi ya ndani (VPL) na mmoja anayecheza nje ambaye ni Nickson Kibabage.

Eneo la golikipa, Kim amemuanzisha Aishi Manula, beki ya kulia amempanga Shomari Kapombe, koshoto Mohamed Hussein huku beki ya kati akimuweka Erasto Nyoni  wote wa Simba pamoja na Dickson Job wa Yanga.

Mudathir Yahya na Salum Abubakar wa Azam pamoja na Kibabage wa Youssoufia Berrechid ya Morocco na Feisal Salum wa Yanga wanacheza kama viungo.

Eneo la ushambuliaji wameanza John Bocco wa Simba na Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar.

Kwenye bechi la Stars wapo, Juma Kaseja, Metacha Mnata, Israel Mwenda, Edward Manyama, Bakari Mwamnyeto, Kennedy Juma,  Meshack Abraham, Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Iddi Seleman, Ayoub Lyanga, Abdul Hamis (wote wa VPL), na Yohana Mkomola anayecheza inhulets ya nchini Ukraine.

Advertisement
Advertisement