Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Palmer amcharukia Jackson, mbioni kupigwa bei

Muktasari:

  • Taarifa zinaeleza kuwa Chelsea wanafikiria kumuuza Jackson endapo tu watapokea ofa ya kuridhisha.

New Jersey, Marekani. Nyota wa Chelsea, Cole Palmer ameonyesha kukerwa hadharani na mchezaji mwenzake Nicolas Jackson baada ya kukosa kupasiwa mpira katika nafasi ya wazi ya kufunga, katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fluminense.

Palmer alikosa uvumilivu katika dakika za lala salama za mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, baada ya Jackson kuamua kupiga shuti badala ya kumpasia akiwa katika nafasi nzuri ya kuunganisha mpira wavuni. Mpira huo uliishia kugonga nyavu za pembeni na kuzua hasira kwa mchezaji huyo wa The Blues, ambaye alinyanyua mikono kwa hasira na kupiga mlingoti wa goli kwa nguvu.

Tukio hilo lilitokea dakika ya 80 ya mchezo ambapo Chelsea walikuwa mbele kwa mabao mawili kupitia mshambuliaji mpya Joao Pedro, aliyefunga mawili dhidi ya timu yake ya zamani.

Pedro, aliyesajiliwa kutoka Brighton kwa pauni milioni 60, alifunga bao la kwanza katika dakika ya 18 kwa shuti kali nje ya boksi, kabla ya kuongeza la pili mwanzoni mwa kipindi cha pili. Licha ya kung’ara, Pedro hakusherehekea kutokana na heshima kwa klabu yake ya zamani ya Fluminense.

Chelsea walipata nafasi ya kuhitimisha mchezo kwa bao la tatu baada ya Jackson, aliyeingia kipindi cha pili kukosa bao la wazi akipiga shuti nje ya lango, jambo lililopelekea Palmer kumkemea kwa sauti huku Jackson akiomba msamaha kwa ishara ya mkono akiwa na uso wa aibu.

Jackson, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Maresca msimu uliopita, sasa anakabiliwa na ushindani mkali baada ya ujio wa Joao Pedro na Liam Delap aliyesajiliwa kutoka Ipswich.

Licha ya kufunga mabao 13 msimu uliopita, mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakimlaumu kwa ukosefu wa nidhamu katika mechi muhimu, akiwemo kutolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Newcastle na tena dhidi ya Flamengo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la Klabu.

Ripoti kutoka Italia zinaeleza kuwa klabu ya AC Milan imeonesha nia ya kumsajili Jackson katika dirisha hili la majira ya joto. Inadaiwa jina la Jackson lilitajwa wakati wa majadiliano kuhusu usajili wa beki wa kushoto wa Gent, Archie Brown, ambaye ana wakala mmoja na Jackson.

Hata hivyo, taarifa hizo zinaeleza kuwa Chelsea wanafikiria kumuuza mshambuliaji huyo endapo tu watapokea ofa ya kuridhisha.

Chelsea sasa inasubiri mshindi kati ya Paris Saint-Germain na Real Madrid watakaokutana nao kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Klabu itakayopigwa Jumapili hii.