Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Partey afikishwa tena mahakamani London

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey wakati alipokuwa akishuka kutoka ndani ya gari kuelekea mahakani kwa ajili ya kusikiliza kesi Aprili 13, 2026. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Partey, ambaye kwa sasa anachezea Villarreal, alishtakiwa mwaka jana kwa makosa matano ya ubakaji dhidi ya wanawake wawili pamoja na shtaka la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke wa tatu.

London, England. Kiungo wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey, amefikishwa tena mahakamani jijini London, England na kukana mashitaka mapya mawili ya ubakaji yanayomhusisha mlalamikaji mwingine.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amefikishwa katika Mahakama ya Southwark Crown Court, ambapo alikana mashitaka hayo mapya.

Partey tayari alikuwa anakabiliwa na kesi nyingine akikanusha tuhuma za kuwabaka wanawake wawili na kumshambulia kingono mwanamke wa tatu.

Mwezi Februari mwaka huu, alishtakiwa kwa mashitaka mawili ya ubakaji dhidi ya mwanamke mwingine, anyodaiwa aliyafanya Desemba 2020 jijini London.

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey, ambaye kwa sasa anaitumikia Villarreal ya Hispania. Picha na Mtandao

Wakili wake, Jenny Wiltshire, amesema mteja wake anaendelea kukataa tuhuma zote na amekuwa akishirikiana na polisi tangu uchunguzi uanze.

Ameongeza kuwa kutokana na kesi hiyo kuwa mahakamani, hawatatoa maelezo zaidi kwa sasa.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, ukiongozwa na Arabella MacDonald, mlalamikaji mpya alijitokeza baada ya taarifa za kesi nyingine za Partey kusambaa kwenye vyombo vya habari.

Partey, ambaye kwa sasa anachezea Villarreal, alishtakiwa mwaka jana kwa jumla ya makosa matano ya ubakaji dhidi ya wanawake wawili pamoja na shtaka la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke wa tatu, kufuatia uchunguzi wa polisi.

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey wakati alipokuwa akicheza katika timu hiyo ya London Kaskazini. Picha na Mtandao

Anatarajiwa kusikilizwa kesi hiyo mwezi Novemba katika mahakama hiyo hiyo, huku akiwa tayari amekanusha mashtaka yote yanayomhusu.

Licha ya kesi hiyo, masharti ya dhamana hayamzuii kuendelea kucheza soka. Hata hivyo, anatakiwa kuwajulisha polisi saa 24 kabla ya kusafiri nje ya nchi na haruhusiwi kuwasiliana na walalamikaji.

Partey aliwahi kujiunga na Arsenal mwaka 2020 akitokea Atletico Madrid kwa ada ya paundi 45 milioni (Sh158 bilioni) na alicheza mechi 167 ndani ya misimu mitano kabla ya kuondoka mwaka jana. Pia anaendelea kuitumikia timu ya taifa ya Ghana na huenda akashiriki michuano ya Kombe la Dunia ijayo itakayofanyika Marekani, Canada na Mexico.